• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
KWA KIFUPI: Chanjo ya kukabiliana na aina mpya ya corona kuwa tayari kufikia Desemba

KWA KIFUPI: Chanjo ya kukabiliana na aina mpya ya corona kuwa tayari kufikia Desemba

Na LEONARD ONYANGO

CHANJO ya kukabiliana na aina mpya ya virusi vya corona itakuwa tayari kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2021.

Kampuni ya AstraZeneca iliyotengeneza chanjo ya corona kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Oxford, inasema kuwa imeanza mikakati ya kutengeneza chanjo nyingine kutokana na hofu kwamba aina mpya ya virusi vya corona huenda vikalemea chanjo inayotumika sasa.

“Tutatengeneza chanjo nyingine yenye nguvu ya kushinda aina mpya ya virusi vya corona. Virusi vya corona hujibadilisha mara kwa mara na kuna uwezekano kwamba chanjo inayotumiwa sasa huenda ikashindwa kufanya kazi katika siku za usoni,” akasema mkuu wa AstraZeneca, Mene Pangalos.

Kwa sasa kuna aina tatu za virusi vya corona ambavyo vimegunduliwa katika mataifa mbalimbali duniani.

Aina ya virusi vya corona inayojulikana kama B.1.1.7 iligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza, B.1.351 vilipatikana kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini na P.1 nchini Brazil.

Mwezi uliopita, Kenya ilitangaza kuwa raia wawili wa kigeni walipatikana na virusi vya B.1.351 humu nchini.

You can share this post!

PATA USHAURI WA DKT FLO: Kiharusi cha muda huletwa na nini?

Jinsi miiba ya ‘Mathenge’ inavyoangamiza...