• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
LISHE: Rosti ya maini

LISHE: Rosti ya maini

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa :Dakika 10

Muda wa Mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Unahitaji

  • maini ya ng’ombe kilo moja
  • kitunguu saumu
  • tangawizi iliyomenywa na kupondwa –kijiko 1
  • kitunguu maji 1
  • chumvi
  • mafuta ya kupikia
  • biringanya 1
  • pilipili mboga 1
  • karoti 1
  • nyanya 2
  • tui la nazi

Maelekezo

Katakata maini yawe vipande vidogo na kisha vioshe vipande hivyo halafu chuja maji na uweke kwenye sufuria.

Weka sufuria mekoni na uashe moto. Ongeza chumvi na mchanganyiko wa kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa.

Acha maini yachemke, ongeza maji moto pale yanapokaukia mpaka yaive kabisa.

Epua maini yako tayari kwa kuyaunga.

 

Chukua sufuria safi, weka kwenye moto, ongeza mafuta ya kupikia na acha yachemke kiasi kisha ongeza chumvi.

Ongeza vitunguu maji na vipike mpaka vibadilike rangi kisha ongeza mchanganyiko wa vitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa.

Ongeza pilipili mboga na biringanya na koroga taratibu na viache viive.

Chukua karoti iliyokatwakatwa na viazi mviringo ambavyo utakuwa umevichemsha kidogo viongezee kwenye sufuria yako.

Ongeza maini yaliyochemka, pamoja na viungo unavyopendelea.

Ongeza nyanya na uache iive ili kutengeneza rojo.

Ongeza tui la nazi na koroga bila kuacha mpaka utakapoona linataka kuchemka, ila hakikisha tui halikatiki kwa kuchemka.

Epua maini yako tayari kwa kuliwa.

  • Tags

You can share this post!

Scotland na Uholanzi nguvu sawa kirafiki

Vuguvugu la Linda Katiba halitachoka kunusuru nchi – Karua