• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
NDIVYO SIVYO: Upatanisho wa kisarufi unavyowatatiza wengi

NDIVYO SIVYO: Upatanisho wa kisarufi unavyowatatiza wengi

NA NYARIKI NYARIKI

KUTOPATANISHWA vyema kwa tungo kisarufi ni mojawapo ya makosa ambayo hujidhihirisha aghalabu katika lugha ya Kiswahili.

Kosa hilo halifanywi tu na wanafunzi au watu wanaojifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili, bali pia baadhi ya watumizi wa lugha hiyo wenye uzoefu mkubwa.

Nimewahi kulichanganua kosa la upatanisho wa kisarufi linalohusu majina ya makundi ambapo kiambishi cha upatanisho wa kisarufi kwenye kitenzi kinachofuata jina la makundi hurejelea nomino zinazounda makundi badala ya makundi yenyewe.

Ifahamike hata hivyo kuwa kosa la upatanisho wa kisarufi halihusu tu majina ya makundi, bali linahusisha pia vipengele vingine vya lugha vinavyojitokeza katika tungo.

Mathalani, umewahi kuwasikia baadhi ya watu wakisema:

*Vitu hizi zitachukuliwa kesho. Licha ya watumizi hao kufahamu wingi wa ‘kitu’ kuwa ni ‘vitu’, aina nyingine za maneno zinazotumiwa na nomino hiyo huwapiga chenga.

“Maudhui chafu kwenye muziki udhibitiwe uache kupotosha vijana’’.

Kwenye mada hii ambayo ilijitokeza kwenye chombo kimojawapo cha habari linajitokeza kosa la upatanisho wa sarufi ambalo linaathiri aina mbili za maneno: Neno la kwanza linaloathiriwa ni kivumishi cha sifa ‘chafu’ ilhali la pili ni kitenzi kinachofuata nomino ‘maudhui’.

Nimewahi kuwasikia baadhi ya ‘wataalamu’ wa lugha ya Kiswahili wakitoa madai kuwa watu wanapaswa kusema ‘maji chafu’ bali si maji machafu.

Binafsi sikubaliani na kauli yao kwa kuwa kivumishi ‘chafu’ tofauti na ‘safi’ (hiki cha pili kinatokana na asili ya kigeni) huongezewa kiambishi kutegemea ngeli inayorejelewa.

…YATAENDELEA

  • Tags

You can share this post!

Sibanduki, mke amkalia ngumu mumewe aliyetaka kumfurusha

Karua: Washukiwa wengi wa ufisadi wanaoachiliwa ni wa...

T L