• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Sibanduki, mke amkalia ngumu mumewe aliyetaka kumfurusha

Sibanduki, mke amkalia ngumu mumewe aliyetaka kumfurusha

MKOMANI, MOMBASA

Na JANET KAVUNGA

JUHUDI za jombi wa hapa za kumtimua mkewe ili aoe mpango wa kando ziligonga mwamba mwanadada alipokataa kubanduka na kumtishia vikali.

Jamaa alikasirika mkewe alipomtaka aache kushiriki mipango ya kando alipopata habari jombi alikuwa akitoka na kipusa mmoja.

Badala ya kutii ushauri wa mkewe, jombi alipandwa na za kwao na kumtaka demu kukusanya virago na kurudi kwa wazazi wake.

Alijua kwamba hajui kwani mkewe alisimama na kumfokea vikali akimwambia hawezi kumuachia boma atumie kuburudisha mipango yake ya kando.

“Ikiwa ulidhani ukali wako utanitisha, sahau. Hapa ni kwangu na sibanduki,” mke akacharuka.

“Kamjengee huyo unayetaka kuleta hapa boma lake hukooooo!” Mwanadada alilipuka hadi jamaa akaingiwa na baridi.

***

Ujumbe kutoka kwa ‘ex’ wavunja penzi la miaka

EMBAKASI, NAIROBI

NA LEAH MAKENA

JAMAA wa hapa aliachwa na kidosho aliyekuwa akipanga kufanya naye harusi alipobaini alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake wa kitambo.

Habari zasema kuwa jamaa alipokuwa akirushia mrembo mistari, aliweka mambo wazi kuwa alikuwa na mpenzi waliyeachana kabisa. Hivi majuzi, polo alijipata kwenye chungu moto alipojibu jumbe za ex wake kwani kidosho alipoziona alimchemkia na kumtema.

“Unajibu jumbe za baby mama na ulisema huwa hamuongei? Hii inaonyesha kuwa mnaweza kurudiana, heri nijitoe mapema,” mrembo alisema.

Jamaa alibaki kukadiria hasara kwani juhudi zake za kusihi mrembo warudiane ziliambulia patupu.

  • Tags

You can share this post!

Pasta atoa ushuhuda jinsi alivyoepuka kupata virusi vya...

NDIVYO SIVYO: Upatanisho wa kisarufi unavyowatatiza wengi

T L