• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
MALEZI KIDIJITALI: Kumkinga na hatari ibuka za mtandao

MALEZI KIDIJITALI: Kumkinga na hatari ibuka za mtandao

NA BENSON MATHEKA

USISUBIRI hadi mtoto wako atumbukie kwenye hatari mtandaoni ndipo umfunze jinsi ya kujikinga.

Wazazi wanaofanya hivi huwa wanatelekeza wajibu wao wa kukinga watoto wao na hatari za mtandao ambazo zinaongezeka kila siku.

Kulingana na wataalamu wa malezi dijitali, ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto wake anajua kutambua na kuepuka hatari za mtandao.

“Usingojee hadi mtoto atumbukie kwenye hatari zinazosababishwa na mtandao. Unaweza kukosa kumuokoa. Lakini ukimwandaa mapema atajua jinsi ya kuepuka na kujilinda. Hili ni jukumu ambalo mzazi hawezi na hafai kuepuka,” asema mtaalamu wa malezi dijitali Ian Doras kwenye makala aliyochapisha mtandaoni.

Anafananisha wazazi wanaosubiri watoto kujipata kwenye hatari na mtu anayesubiri hadi nyumba au gari lake livunjwe ili achukue hatua za kuilinda.

“Linda mtoto wako mapema kwa kujifahamisha kwanza na hatari ibuka za mtandao na zilizopo, mshauri vilivyo na uendelee kumkumbusha. Kufanya hivi kutamhakikishia usalama wake, kutamfanya akue akijua hatari zilizopo na kuwafunza wenzake na marafiki. Hii itahakikisha jamii ni salama,” asema Ian na kuongeza kuwa wahalifu wa mtandao wanabuni mbinu salama kila siku za kulenga watoto na watu wasio na habari.

“Kwa kuwa wahalifu wanabuni mbinu mpya kila wakati, mzazi hana budi kuwa mwangalifu zaidi, kujifahamisha na hatari ibuka ili kuwa katika nafasi nzuri ya kulinda mtoto wake,” asema Ian.

Kulingana na Deborah Cox, mwanasaikolojia na mtafiti wa masuala ya usalama wa watoto, njia ya pekee ya wazazi na walezi kuhakikishia watoto wao usalama wa mwili na akili sio kuwanyima mtandao na vifaabebe mbali ni kuwatambulisha mapema, kuwaelekeza na kuwashauri ipasavyo.

“Usimnyime mtoto wako mtandao na vifaabebe. Mtambulishe mapema na uendelee kumfunza na kumshauri kuhusu hatari kwa kupalilia urafiki na utakuwa umemfanyia haki,” asema.

You can share this post!

SHANGAZI SIZARINA: Nina wasiwasi kumhusu binti yangu,...

MAPISHI KIKWETU: Nyama ya mbuzi na viazi vilivyopondwa

T L