• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Mama anayefanya ukahaba alivyokutana na mwanawe kwenye lojing’i     

Mama anayefanya ukahaba alivyokutana na mwanawe kwenye lojing’i     

NA MWANGI MUIRURI

Motel, Kirinyaga 

TEKNOLOJIA ya True Caller imemvisha mwanamke mmoja Mjini Thika aibu ya mwaka baada ya kuelekeza mtoto wake hadi lojing’i za mtaa ambapo hujichuuza kimahaba.

Teknolojia hiyo ya True Caller kwa simu huwezesha unaowasiliana nao kujua jina lako kwa mujibu wa jinsi wengine wamekuhifadhi kwa simu zao.

Lakini kuepuka balaa, mmiliki wa nambari ya simu huwa na uwezo wa kuweka jina ambalo jinsi angetaka liwe likitumwa kwa anaowasiliana nao, bora simu hiyo ni aina ya smartphone.

“Shida ya mama huyu ni vile hakuwa ameweka jina ambalo angetaka liwe likimfahamisha kupitia kwa True Caller. Hatari ikawa akipigiwa au akipiga simu, jina lililokuwa likijitokeza ni Poko wa Makutano,” akasema mdokezi.

Ukumbi huu ulifahamishwa kuwa mtoto wa kiume wa miaka 19 wa mama huyu wa miaka 45 alitaka kujua ukweli wa nambari ya mamake ya simu kumtambulisha kwa umma kwa jina “Poko”, jina la mtaani la kahaba.

“Kijana huyo aliabiri gari kutoka Mjini Thika hadi Makutano ambapo nauli ni Sh150. Alikuwa ameandamana na rafiki yake kumsaidia kupata ukweli wa mambo,” akasema mdokezi.

Kijana huyo kufika Makutano alimpa rafikiye nambari ya simu ya mamake na akamwelekeza aipige na ajifahamishe kama rafiki anayetaka wakutane.

“Mama kusikia sauti ya mwanamume ndiyo inamtafuta alidhania ni mteja wa mahaba na akamwelekeza hadi lojing’i ambapo makahaba huwa wamepanga vyumba vya kibiashara,” akasema mdokezi.

Kwa kuwa kwa lojing’i hizo pia huwa na biashara ya pombe, mama alijiweka chonjo ndani ya baa ili mwanamume huyo akifika kwanza anunue kileo huku wakijadiliana biashara ya mahaba.

“Huku akiwa amevalia nusu uchi matiti na mapaja yakiwa nje na makalio yakiwa yamebanwa kiasi cha kukaa kama mchoro, alikaa akingoja mpigaji simu aingie,” mdokezi asema.

Na mwanamume aliingia akiandamana na yule kijana wake na ndipo hali ikageuka kuwa balaa.

“Kumbe mamangu ulihepa kwa babangu ili utulee mimi, kakangu na dadangu kupitia pesa za ukahaba? Ukahepa kanisani ili uhamie ndani ya lojing’i ukiwa unavaa hivi aibu isiyowiana na mama wa miaka 45?” Mtoto akafokea mamake.

Wahudumu wa lojing’i hizo waliingilia kati na wakampeleka mwana na mamake pembeni wakajadiliane ya kwao nyumbani na kifamilia pasipo kujianika kwa umma.

“Hatimaye mwana na mamake walionekana wakitoka kwa lojing’i hiyo na wakafululiza hadi kwa steji na kuabiri gari la kuelekea Thika…Kwa sasa ni wiki imeisha na huyo mama hajakanyaga hapa,” akasema mdokezi wetu.

Hali hiyo iliwahamasisha makahaba wengine kuingia kwa simu zao na kufanyia uhariri majina yao kwa True Caller lakini wale ambao hawana simu pevu aina ya smartphone bado wakibakia katika hatari ya kuanikwa.

“Itabidi ukiwa katika biashara haramu utumie nambari ambayo haijulikani katika familia yako na pia wandani wengine ili ujiepushe na hatari ya True Caller kukuandalia aibu ya mwaka,” akasema mmoja wa mteja katika lojing’i hizo.

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Mmiliki tapeli wa shule  

Karisa Nzai ateuliwa kama msemaji wa Mijikenda

T L