• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
MAPISHI KIKWETU: Biriani ya Uyoga

MAPISHI KIKWETU: Biriani ya Uyoga

NA PAULINE ONGAJI

Viungo

  • Uyoga kilo – 1
  • Mchele wa basmati, kilo – 1
  • Masala, vijiko via chai – 4
  • Kitunguu saumu kilichokatwa kwa vipande vidogo, vijiko vya chai – 4
  • Siagi au samli, gramu – 50
  • Mdalasini uliokatwa kwa vipande vidogo, vijiko vya chai – 4
  • Vitunguu vilivyokatwa kwa silesi nyembamba, kikombe – 1
  • Pilipili mboga iliyokunwa, vijiko vya chai – 3
  • Dhania kifungu – 1
  • Mafuta ya mboga ya kukaanga, vijiko vya meza – 5
  • Maziwa lala, vikombe – 2
  • Nyanya zilizokunwa, kikombe – 1
  • Chumvi na pilipili, kwa ladha

Jinsi za kutayarisha
1. Chemsha maji, ongeza unga wa masala, kijiko 1/2 pamoja na mchele.
2. Pika mchele, lakini usive kabisa na kuwa mwepesi. Ondoa maji yaliosalia kisha uuweke mchele kando.
3. Huku kiwango cha moto kikiwa cha chini, tia mafuta ya kukaanga kwenye sufuria nzito.
4. Ongeza vitunguu, kaanga hadi vionekane kubadili na kuwa rangi ya hudhurungi hafifu.
5. Tia masala vijiko 2, pamoja na viungo vingine vyote, ikiwa ni pamoja na nyanya, lakini sio mchele.
6. Pika kwa dakika 5, kisha uongeze uyoga.
7. Endelea kupika hadi uyoga uive na kuwa laini
8. Tia kitoweo cha uyoga kwenye mchele kisha unyunyize kijiko 1 cha unga wa masala, siagi au samli
9. Ukitumia karatasi maalum ya kufunikia chakula, funika sufuria, kisha upunguze kiwango cha moto hadi cha chini. Pika kwa dakika 10 – 15 zaidi. Andaa wali ukiwa mmoto.

You can share this post!

MALEZI KIDIJITALI: Kuepushia mtoto wako kutekwa na...

UJAUZITO NA UZAZI: Kukabili uvujaji damu baada ya kujifungua

T L