• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 8:50 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Kukabili uvujaji damu baada ya kujifungua

UJAUZITO NA UZAZI: Kukabili uvujaji damu baada ya kujifungua

NA PAULINE ONGAJI

… Imeendelea

Ishara

  • Kutokwa na majimaji mekundu kutoka ukeni kwa zaidi ya siku saba baada ya kujifungua
  • Kutokwa na majimaji yanayotoa harufu mbaya
  • Homa na kuwashwa
  • Kuvuja damu kusiko kwa kawaida (ambapo kisodo kizito kinalowa chini ya saa moja)

Ni nini kinachosababisha hali hii?

  • Kwa mara nyingi hali hii hutokea wakati nyungu ya uzazi inapokosa kurejea hali yake ya kawaida baada ya kujifungua. Hii husababisha sehemu hii kuendelea kuvuja. Mambo mengine yanayosababisha hali hii ni pamoja na:
    o Kukosa kuondoka kwa mji wote baada ya kujifungua
    o Kutolewa kwa mji kwa nguvu
    o Majeraha kwa nyungu ya uzazi, njia ya uzazi au uke wakati wa kujifungua

Kila mwanamke yuko katika hatari ya kukumbwa na shida hii, lakini kuna sababu zingine zinazoongeza uwezekano wa kuathirika, kama vile:

  • Kujifungua zaidi ya mtoto mmoja ka wakati mmoja
  • Placenta previa, hali inayotokea wakati mji unaposhikana na ukuta wa nyungu ya uzazi kiwango cha kufunika njia ya uzazi. Hali hii hutokea sana wakati wa kujifungua mtoto wa pili.
  • Uchungu wa kuzaa uliochochewa
  • Kumzaa mtoto mkubwa

Hali hii hutibiwa vipi?

  • Kukandwa katika sehemu ya chupa ya uzazi ili kusisimua misuli na hivyo kupunguza kuvuja kwa damu
  • Matumizi ya dawa zinazopunguza kuvuja damu kuambatana na ushauri wa daktari
  • Kuoundolewa kwa mji uliyosalia kwa kutumia mkono
  • Kuongezewa damu
  • Kuondolewa kwa chupa ya uzazi iwapo imeharibika.

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Biriani ya Uyoga

AC Milan wakomoa Juventus katika Serie A na kuweka kocha...

T L