• Nairobi
 • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
MAPISHI KIKWETU: Kuku choma, paprika, mdalasini na dengu

MAPISHI KIKWETU: Kuku choma, paprika, mdalasini na dengu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

DENGU ni mbegu za jamii ya kunde na zipo katika rangi mbalimbali zikiwemo nyekundu, kijani kibichi, kahawia, njano na nyeusi.

Dengu zina nyuzinyuzi nyingi, folati na potasiamu na kuzifanya kuwa chaguo bora kwa moyo na kudhibiti shinikizo la damu na lehemu. Pia ni chanzo cha madinin ya chuma na vitamini B1 ambayo husaidia kudumisha mapigo ya moyo.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • dengu za kahawia kikombe 1 ½
 • vikombe 3 vya mchuzi kutokana na nyama ya kuku
 • mtindi wa Kigiriki kikombe ¾
 • kijiko 1 cha maji ya limau
 • paprika kiijiko 1 ½
 • jira kijiko 1 ½
 • kijiko 1 cha poda ya vitunguu
 • kijiko 1 cha chumvi ya baharini yaani sea salt
 • kijiko ½ cha mdalasini
 • nyama nzima ya kuku
 • karoti 5 kubwa, katakata vipande.
 • kijiko 1 cha chumvi
 • vijiko 2 vya pilipili nyeusi
 • majani ya giligilani

Maelekezo

Washa ovena hadi nyuzijoto 200 kwa dakika 10.

Katika sufuria, changanya dengu na supu kutokana na nyama ya kuku. Chemsha juu ya moto mwingi na upike kwa dakika 10.

Katika kijibakuli, changanya mtindi, maji ya limau, paprika, jira, unga wa vitunguu, chumvi na mdalasini. Koroga na kuchanganya vizuri.

Pangusa kuku kipande kiwe kikavu kabisa ndani na nje. Nyunyizia mchanganyiko wako kwenye kuku kote, ndani na nje, na chumvi na pilipili.

Paka kuku mzima na robo ya kikombe cha sosi ya mtindi. Weka kuku juu ya dengu katika chombo cha kuokea na upange karoti karibu na kuku.

Oka kuku kwa dakika 30. Anza kuangalia utayari wako zikibaki dakika 10. Ruhusu kuku kupumzika kwa dakika 10.

Ongeza sosi wa mtindi uliobaki kwenye sinia. Kijiko cha lenti juu ya mtindi, kisha kuongeza karoti na kuku.

Nyunyizia majani ya giligilani kwa juu kabla ya kupakua na kufurahia.

 • Tags

You can share this post!

SJAK na LG wasaini kandarasi ya Sh3.5m kutuza wanamichezo...

Fahamu jinsi ya kuoka mkate wa Zucchini

T L