• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 AM
Fahamu jinsi ya kuoka mkate wa Zucchini

Fahamu jinsi ya kuoka mkate wa Zucchini

NA MARGARET MAINA

[email protected]

ZUCCHINI huwa na virutubisho vingi. Ingawa zucchini mara nyingi huchukuliwa kuwa mboga, huainishwa kibotania kama tunda. Zifuatazo ni baadhi ya sifa za zucchini.

  • virutubisho vingi
  • huimarisha usagaji wa chakula mwilini
  • husaidia kuimarisha maono yako
  • kupunguza viwango vya sukari kwenye damu
  • kuboresha afya ya moyo
  • kusaidia kupunguza uzito
  • rahisi kuongeza kwenye mlo wako

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

kikombe 1 zucchini.

kikombe 1 cha karoti (menya na saga)

siagi kikombe ½ (iliyoyeyuka)

kikombe ¼ cha sukari nyeupe

kikombe ½ cha sukari ya kahawia

mayai 2

dondoo la vanilla kijiko 1

kikombe 1 ½ unga wa ngano

mdalasini kijiko 1

baking soda kiasi cha kijiko 1 cha kukorogea chai

kijiko ½ cha chumvi

kikombe cha karanga (kilichokatwa)

kikombe nusu chipsi tamu za chokoleti (hiari)

Hatua mojawapo ya kuoka mkate wa Zucchini. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Osha na suuza Zucchini na karoti.

Koroga kwa pamoja zucchini, karoti, siagi iliyopozwa (iliyoyeyuka), sukari, mayai, na vanilla.

Katika bakuli jingine, changanya unga wa ngano, mdalasini, soda ya kuoka na chumvi.

Changanya viungo kavu na mchanganyiko wa zucchini. Koroga hadi vichanganyike tu.

Kisha koroga karanga na chokoleti, ikiwa unatumia.

Mimina unga kwenye sufuria ya kuokea mkate iliyopakwa siagi.

Oka kwa digrii 180 kwa muda wa dakika 40 hadi uma ukiingizwa katikati utoke ukiwa safi.

Subiri mkate upoe kabla ya kula.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Kuku choma, paprika, mdalasini na dengu

Serikali yazuia maziwa ya Kenyatta kutoka Uganda kuingia...

T L