• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 10:55 AM
MAPISHI KIKWETU: Matoke na nyama ya mbuzi iliyokaangwa

MAPISHI KIKWETU: Matoke na nyama ya mbuzi iliyokaangwa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 3

Vinavyohitajika

kilo 1 nyama ya mbuzi

punje 4 kitunguu saumu; sagasaga

kijjiko ½  cha thyme

juisi ya limau

mtindi

kijiko 1 cha sosi ya soya

ndizi 15 za kijani kibichi (zimechujwa na kukatwa vipande vipande)

nyanya 3

maji

vitunguu maji 2, katakata vipande vipande

majani ya giligilani

pilipili mboga

chumvi

mafuta ya kupikia

Ndizi mbichi. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Changanya mtindi wako wa kawaida, sosi ya soya au uyoga, thyme na maji ya limau.

Baada ya yote kuchanganywa, ongeza kitunguu saumu chako kilichosagwa na uchanganye. Mara baada ya kusambazwa sawasawa, mimina yaliyomo kwenye nyama yako ya mbuzi iliyokatwa na uiruhusu ikae kwa si chini ya muda wa saa tatu.

Weka nyama pamoja na mchanganyiko wako kwa sufuria mekoni ili vichemke kwa pamoja. Usiioshe nyama maana kwa kuacha hivyo itageuka kuwa nzuri na yenye ladha zaidi. Ongeza kikombe 1 cha mchuzi wa nyama ya nyama ya ng’ombe/ mboga au maji kidogo ili kuhakikisha nyama inakuwa laini.

Baada ya nyama kuchemka, weka kando. Katika kikaango tofauti, ongeza vitunguu, tangawizi na pilipili na kaanga. Vitunguu vyako vikishakuwa laini, weka nyanya yako kisha vikaange kwa takribani dakika tano au hadi vilainike.

Ongeze nyama, changanya, kisha, ongezea viungo upendavyo. Funika na baada ya dakika tano, epua.

Chemsha ndizi kwa dakika 15, kisha zikaange kwa mafuta na kitunguu na nyanya.

Ongezea mtindi na ufunike kisha uache chakula kiive kwa dakika tano hivi.

Ongezea majani ya giligilani kwa juu, epua na upakue. Furahia chakula chako.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Mchuzi wa njegere na viazi mbatata

Bunge la Mwananchi lakosoa agizo la Koome washukiwa wa...

T L