• Nairobi
 • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Pilipili ya limau kwa kuku choma huongeza ladha

MAPISHI KIKWETU: Pilipili ya limau kwa kuku choma huongeza ladha

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 3

Vinavyohitajika

 • kilo mbili nyama ya kuku halafu ikatwe vipande
 • vijiko 2 vya chumvi
 • vijiko 3 vya mafuta ya mboga
 • vijiko 4 jibini ya pamesan
 • vitunguu maji 2 vilivyokatwa vipande vyembamba
 • punje 4 za vitunguu saumu viliyokatwa
 • iliki
 • haradali
 • kijiko 1 cha zest ya limau kutoka kwa limau 1
 • vijiko 2 vya paprika
 • kijiko 1 cha poda ya vitunguu saumu
 • kijiko 1 cha unga wa vitunguu
 • kijiko cha udaha
 • kijiko 1 cha pilipili nyeusi

Maelekezo

Tengeneza kitoweo cha viungo vya pilipili ya limau. Katika bakuli kubwa changanya zest ya limau, chumvi, paprika, poda ya vitunguu saumu, poda ya vitunguu, udaha, na pilipili nyeusi hadi vichanganyike vizuri.

Tenga kijiko kimoja cha kitoweo cha pilipili ya limau utakayoyachanganya na sosi ya pilipili ya limau utakayotayarisha baadaye.

Kausha nyama za kuku kwa kitambaa cha karatasi na uzitumbukize kwenye bakuli kubwa lenye kitoweo cha pilipili ya limau na koroga hadi nyama iwe imechanganyika sawasawa.

Tengeneza mchuzi wa pilipili ya limau. Katika bakuli ndogo, changanya pamoja mayonesi, mtindi, asali, haradali, zest ya limau, maji ya limau, vitunguu, pilipili nyeusi na iliyohifadhiwa kisha kijiko kimoja cha mchanganyiko wa viungo.

Changanya mpaka viwe laini. Chota mchuzi nusu kikombe na uongeze kwenye bakuli lenye nyama ya kuku. Changanya tena mpaka kuku kuchanganyika kisawasawa kwenye marinade.

Washa grili lako kwa moto wa juu. Paka mafuta kwenye chombo cha grili. Weka nyama kwenye grili na upike, ukizungusha mara kwa mara, hadi ngozi iwe kahawia ya dhahabu na kuku kuiva vizuri. Itakuchukua muda wa dakika 30.

Hamisha nyama zilizochomwa kwenye sinia na nyunyuzia jibini iliyokunwa ya Parmesan na majani ya giligilani, ikiwa unatumia. Ongeza pilipili nyeusi zaidi ikiwa utapenda.

Tumia mchuzi wa pilipili ya limau iliyobaki kando ya kuchovya. Furahia.

 • Tags

You can share this post!

Man-City sasa yatangazia Arsenal hali ya hatari EPL

Wakristo waonyesha undugu na Waislamu wakati wa Ramadhani

T L