• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
MAPISHI KIKWETU: Saladi ya karoti na mananasi

MAPISHI KIKWETU: Saladi ya karoti na mananasi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

NANASI lina virutubisho vingi vyenye manufaa pamoja na vitamini C, manganisi, na vimeng’enya vya kusaidia usagaji chakula.

Virutubisho

Mananasi yana kalori chache lakini yana sifa ya kuvutia ya virutubisho. Pia yana kiasi kidogo cha fosforasi, zinki, kalsiamu, na vitamini A na K.

Vitamini C ni muhimu kwa afya ya kinga, unyonyaji au ufyonzaji wa madini ya chuma, na ukuaji wa seli, wakati manganisi ni muhimu katika usawazishaji wa mifanyiko ya kimetaboliki.

Karoti nazo ni chanzo kizuri hasa cha Beta carotene, nyuzinyuzi, vitamini K1, na madini ya potasiamu. Karoti ni chakula kizuri cha kusaidia kupunguza uzito na kinahusishwa na viwango vya chini vya lehemu pamoja na kazi muhimu ya kuboresha afya ya macho.

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • Mafuta ya mzeituni
  • Karoti 4
  • Sultana, gramu 250
  • Nanasi kilo 1

Maelekezo

Chambua na usafishe karoti.

Kata karoti kwa kutumia kikunio na uweke kando.

Osha nanasi uondoa sehemu ya juu yenye miba halafu ulikate kwenye kete au vipande vidogo.

Changanya karoti, vipande vya nanasi na sultana kwenye bakuli.

Nyunyizia mafuta ya mzeituni juu ya saladi na uchanganye.

Weka saladi kwenye jokofu iwe baridi kiasi kabla ya kupakua na kufurahia.

  • Tags

You can share this post!

Akothee na Andrew Kibe wakabana koo

Vijana wakongamana Thika kwa mawaidha, michezo

T L