• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
MAPISHI: Maharagwe yenye tui la nazi

MAPISHI: Maharagwe yenye tui la nazi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa upishi: Saa moja na nusu

Walaji: 3

Vinavyohitajika

· maharage kilo nusu

· tui nzito kikombe 1

· kitunguu saumu kilichotwangwa kijiko 1

· kitunguu maji kilochokatwa

· pilipili mboga iliyokatwa

· karoti iliyoparwa

· chumvi kijiko 1

· mafuta ya kupikia vijiko 2

· Royco kijiko 1

· nyanya zilizosagwa 3

· maji kiasi ya kuchemshia

Utaratibu

Safisha maharagwe uondoe uchafu wote na uyaoshe vizuri.

Maharagwe safi kabla ya kupikwa. Picha/ Margaret Maina

Yaweke maharagwe kwenye sufuria kisha ongeza maji.

Funika sufuria kisha chemsha maharagwe mpaka maji yapungue.

Sasa weka maji kidogo kidogo ila yasifunike maharagwe yako ili yaive.

Katika sufuria nyingine, weka mafuta na uache yapate moto.

Weka vitunguu maji uvikaange lakini hakikisha haviungui.

Ongeza pilipili mboga na ukaange vizuri.

Weka karoti na uendelee kukaanga.

Ni muhimu pia uweka kitunguu saumu huku ukiendelea kukaanga.

Ukishafanya hivyo, mimina nyanya zilizo sagwa kisha koroga mchanganyiko wako.

Weka chumvi na Royco kisha funika acha ichemke kwa dakika moja.

Mimina maharagwe na uyaache kwa dakika moja.

Kisha mimina tui acha lichemke kwa dakika tatu.

Mimina tui kisha yakoroge maharagwe yako kidogo halafu uyaache yachemke kwa dakika mbili.

Epua lakini acha muda wa dakika tano hivi ndipo uyapakue.

Unaweza kula ama na wali, ugali au slesi za mkate.

MUHIMU:

Hakikisha maharagwe yanaiva vizuri  na ili maharagwe yawe mazito hakikiksha yanapoa kidogo kabla uyapakue.

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa visheti

Makazi ya kocha Ancelotti yavamiwa mjini Merseyside,...