• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Siku 10 za mwanzo za mwezi muhimu wa Dhul Hijja

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Siku 10 za mwanzo za mwezi muhimu wa Dhul Hijja

NA HAWA ALI

SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Subuhaanahu wata’ala, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

Swala na salamu zimwendee mtume wetu Muhammad swalla Allahu a’alayhi wasallam, swahaba zake kiram na watangu wote wema wote hadi siku ya kiyamaah.

Miongoni mwa misimu maalumu ya ibada ni siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah, ambazo Mwenyezi Mungu amezipendelea kuliko siku nyingine zote za mwaka.

Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake) kwamba, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo matendo mema yanazidi kupendwa na Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi kumi.”

Watu wakauliza, “Hata Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu?” Akasema. “Hata Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ila kwa mtu aliyetoka kupigana, akijitolea nafsi yake na mali yake kwa ajili ya jambo hilo, na akarudi bila kitu.” (Imepokelewa na al-Bukhari).

Mwenyezi Mungu anaapa kwa hizi siku, na kuapa kwa kitu ni dalili ya umuhimu wake na faida kubwaSiku kumi hizi ni pamoja na Siku ya Arafa, ambayo Mwenyezi Mungu aliikamilisha Dini yake. Kufunga siku hii itafutiwa madhambi ya miaka miwili.

Muislamu afanye nini katika siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah?

Saumu ni miongoni mwa matendo bora kabisa. Mtume (S.A.W) alikuwa akifunga siku ya tisa ya Dhul-Hijjah

Muislamu pia anahimizwa afunge siku nyingi zilizobakia, isipokuwa siku ya Arafa.

Ni Sunna kusema takbir, tahmid, tahlil, na tasbih katika siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah, na kuitamka kwa sauti kubwa msikitini, nyumbani, barabarani na kila sehemu inaporuhusiwa.

Kuhiji na Umra mi moja ya amali bora anazoweza kufanya mtu katika siku hizi

Kutenda mema zaidi kwa ujumla wake: kama vile kuabudu, kuswali, kusoma Qur’ani, kumdhukuru Mwenyezi Mungu, kuomba dua, kutoa sadaka,kuwafanyia wema wazazi, kudumisha mafungamano ya jamaa, kuamrisha mema na kukataza maovu.

Kuchinja mnyama kama vile mbuzi, kondoo, ng’ombe, ngamia siku ya idi.

Toba ya kweli.

  • Tags

You can share this post!

Tetemeko laua watu 1,000 Afghanistan

Hoki: Mechi 3 kupigwa Jumapili

T L