• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
MIZANI YA HOJA: Tanzania ‘yaharamisha’ matumizi ya Kiswahili kuimarisha Kiingereza

MIZANI YA HOJA: Tanzania ‘yaharamisha’ matumizi ya Kiswahili kuimarisha Kiingereza

NA BITUGI MATUNDURA

SERIKALI ya Tanzania ‘imepiga marufuku’ matumizi ya Kiswahili katika shule za sekondari ili kuimarisha taaluma.

Afisa wa Elimu katika Mkoa wa Mara, Bw Benjamin Oganga alisema: “Katika kuimarisha taaluma, tumetoa maelekezo, kwa Mkoa wa Mara, kuanzia taraehe 9, Januari 2023, wanafunzi wote ambao wataanza (masomo ya) kidato cha kwanza, wataanza na English Orientation kwa kipindi cha wiki nane. Na tutawatest wanafunzi wale,” akatanguliza.

“Hakuna kusoma masomo ya kawaida. Watafanya English Orientation, baada ya wiki nane, tutawatest wanafunzi, na tutajua viwango vyao vya uelewa wa Kiingereza. Na la tatu katika hilo, tumepiga marufuku, lugha ya Kiswahili kutumika, kwenye shule zetu zote za sekondari,” akasema Bw Oganga.

“Tunahitaji kuhakikishe kuwa wanafunzi wanamudu lugha ya Kiingereza, kama ambavyo sera ya elimu na sheria ya elimu inavyoelekeza. Tumebaini kuwa, lugha ile, inasababisha wanafunzi wengi kufeli kwa sababu hawamudu namna ya kuweza kujieleza,”akaelezea.

Mgoda wa Kigoda cha Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Aldin Mutembei, aliwauliza wataalamu wa Kiswahili katika ukumbi wa WhatsApp wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU): “Nisaidieni waungwana. Sheria na Sera ya Elimu (Tanzania) inasema nini kuhusu Kiswahili?”

Prof F.E.M.K Senkoro alijibu kwa bezo: “Yaani natamani kukutana na huyu ndugu (Bw Oganga) tutunishiane misuli kitaaluma.”

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Kabianga kuwa mwenyeji wa Kongamano la 21 la...

NGUVU ZA HOJA: Nina matumaini matumizi ya Kiswahili katika...

T L