• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
NGUVU ZA HOJA: Nina matumaini matumizi ya Kiswahili katika Seneti yataendelea kushika kasi

NGUVU ZA HOJA: Nina matumaini matumizi ya Kiswahili katika Seneti yataendelea kushika kasi

NA PROF IRIBE MWANGI

MAPEMA juma hili, nilimsikia Naibu Spika wa Seneti Mhe Kathuri Murungi akizungumza kuhusu matumizi ya Kiswahili katika Seneti na nikachangamka mno.

Alikuwa akizungumza katika ibada ya madhehebu anuai iliyohudhuriwa na Rais William Ruto katika Kaunti yangu ya Laikipia.

Katika mazungumzo hayo, Naibu Spika alimsifu Seneta wangu, John Kinyua, kwa kuwa mweledi wa kanuni za Seneti, mwenye hoja nzito na mtumizi bora na fasaha wa lugha ya Kiswahili.

Seneta Kinyua alikuwa mmoja kati ya Maseneta waliopenda kuwasilisha hoja zao kwa Kiswahili katika Seneti ya awamu ya pili kwa mujibu wa Katiba inayotumika.

Alikuwa katika kundi dogo lililojumuisha maseneta kama vile Isaac Mwaura na Agnes Zani kati ya wengine.

Kwa hakika, nilikuwa na tashwishi kuhusu matumizi ya Kiswahili katika Seneti baada ya uchaguzi kwa kuwa baadhi ya wapiganiaji mashuhuri wa Kiswahili kama Seneta Mwaura na Seneta Zani walikuwa hawarejei katika Seneti ya awamu ya tatu.

Nilihisi kwamba lugha ya Kiswahili ilikuwa imepoteza. Naukumbuka mchango maridhawa alioutoa Mhe Mwaura katika vikao vyetu wakati tukitafsiri Kanuni za Kudumu za Seneti zinazotumika sasa.

Hata hivyo, matukio yaliyofuatia yalipunguza hofu niliyokuwa nayo. Katika kikao cha kwanza, Spika wa Seneti Gavana Amason Kingi alitumia Kiswahili katika mawasilisho yake.

Maseneta wengi walikula kiapo kwa Kiswahili. Mhe Kathuri amekiri kuwa matumizi yake ya Kiswahili ni jambo la hiari na kiuteuzi.

  • Tags

You can share this post!

MIZANI YA HOJA: Tanzania ‘yaharamisha’ matumizi ya...

GWIJI WA WIKI: Laura Rua

T L