• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
NGUVU ZA HOJA: Kabianga kuwa mwenyeji wa Kongamano la 21 la Kimataifa la CHAKITA

NGUVU ZA HOJA: Kabianga kuwa mwenyeji wa Kongamano la 21 la Kimataifa la CHAKITA

NA PROF JOHN KOBIA

MOJAWAPO ya masuala yanayoathiri dunia kwa sasa ni mabadiliko ya tabianchi.

Kwa hakika mojawapo ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ni suala la mabadiliko ya tabianchi, hasa uhifadhi wa mazingira na kuongezeka kwa viwango vya halijoto. Lugha na Fasihi zina nafasi ya kusawiri masuala haya.

Ni kutokana na hali hii ambapo Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kabianga kitaandaa Kongomano la Kimataifa la Kiswahili kuanzia Machi 1 hadi 2 mwaka huu 2023.

Kongamano litafanyika katika Chuo Kikuu cha Kabianga, kilicho karibu na mji wa Kericho katika Kaunti ya Kericho.

Akithibitisha haya, Mwenyekiti wa CHAKITA Prof Mark Mosol Kandagor alisema kuwa, “Tunashukuru Chuo Kikuu cha Kabianga kwa kukubali kutualika kuandaa Kongamano la CHAKITA katika chuo hicho. Kongamano litafanyika Machi 1 hadi 2 mwaka huu. Tunawaomba wataalamu wa Kiswahili watume ikisiri zao kabla ya Januari 22, 2023.”

Kongamano hili litakuwa la 23 tangu CHAKITA kibuniwe.

Kaulimbiu au mada kuu ya kongamano la mwaka huu ni Kiswahili na uchumi wa kijani. Kongamano litaangazia mada ndogo kama vile Kiswahili na kilimo, Kiswahili na misitu, Kiswahili na mazingira, lugha na fasihi katika maendeleo endelevu.

Isitoshe, kutakuwa na mada ndogo kama vile Kiswahili na nishati, tafsiri na uchumi wa kijani, lugha na teknolojia ya kijani, Kiswahili na umataifa miongoni mwa nyingine.

Makala elekezi yatatolewa na Prof Kimani Njogu – msomi na mtaalamu wa Kiswahili na utamaduni.

Wataalamu na wasomi wa Kiswahili kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wanatarajiwa kuwasilisha makala katika kongamano hilo.

Kongamano la Kabianga litafungua milango ya makongamano mengi ya Kiswahili mwaka huu.

  • Tags

You can share this post!

MIZANI YA HOJA: Mafanikio katika maisha ni zao la jitihada...

MIZANI YA HOJA: Tanzania ‘yaharamisha’ matumizi ya...

T L