• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Msichana wa miaka 17 aeleza jinsi mradi wake wa kupanda miti unavyofaidi jamii 

Msichana wa miaka 17 aeleza jinsi mradi wake wa kupanda miti unavyofaidi jamii 

NA WINNIE ONYANDO

IVY Mumbi, msichana mwenye umri wa miaka 17 ana mradi wa kupanda miti na kufikia sasa amepanda miti ipatayo 1, 000.

Akiwa na lengo la kuleta mabadiliko katika jamii, Mumbi ameshirikiana na Shule moja ya msingi katika Kaunti ya Kajiado na anatumia mradi wake unaotambulika kama TUNITWA, kufunza wanafunzi umuhimu wa kupanda miti.

“Nafurahi kuhesabika kama mojawapo ya watu wanaoleta mabadiliko katika jamii. Mradi huu niliuanzisha Agosti mwaka huu na kufikia sasa, nimeanza kuona matunda yake,” akasema Mumbi wakati wa mahojiano na Taifa Leo Dijitali.

Kando na kupanda miti, Mumbi pia ameanzisha klabu ya mchezo wa Chess katika shule anayosomea na hata kusambaza sodo bila malipo kwa wasichana wenza.

“Nikiwa na umri mdogo, niliona kwenye televisheni jinsi watu wanavyoteseka kwa sababu ya njaa iliyosababishwa na ukame. Nilimsihi babangu awape misaada na kwa kweli alifanya hivyo. Hii ilinipa motisha kuanzisha miradi yangu ya kuwasaidia watu wasiojiweza.

“Mradi huu pia ni njia mojawapo kufunza watoto kuwa katika mstari wa mbele kuleta mabadiliko katika jamii,” akaongeza Mumbi.

Msichana Mumbi alikuwa miongoni mwa washirika watano waliokuwa wakionyesha miradi yao kwenye onyesho la TED (Teknolojia, Burudani, na Ubunifu) katika Shule ya Brookhouse jijini Nairobi.

Hata hivyo, anahimiza serikali ya Kenya Kwanza kuendeleza mchakato wa kupanda miti akisema kwamba nchi inapiga hatua hasa katika kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Naamini kwamba serikali inapiga hatua kubwa. Niliona Rais William Ruto akihimiza Wakenya kukumbatia magari ya kielektroniki. Kando na hayo, aliongoza katika mpango wa upandaji miti. Hii ni ishara tosha kwamba tunapiga hatua.”

Naye mlezi wa programu hiyo Joyce Gacheru, alisema kwamba onyesho hilo linawapa wanafunzi fursa ya kuchangia masuala yanayokumba ulimwengu kama vile mabadiliko ya tabianchi.

Novemba 13, 2023 Rais Ruto aliongoza nchi katika upanzi wa miti.

Siku hiyo zaidi ya miche milioni 150 ilipandwa, hii ni kulingana na msemaji wa serikali Isaac Mwaura.

Aidha, serikali inalenga kupanda miche bilioni 15 kufikia 2023, hatua hii ikiwa mojawapo ya mbinu kukabiliana na athari hasi za tabiachi.

  • Tags

You can share this post!

Atwoli achaguliwa tena kama Rais wa Muungano wa Vyama vya...

Madereva wa matrela ya masafa marefu walaumiwa kwa...

T L