• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
MUME KIGONGO: Damu kwenye mkojo inaweza kuwa dalili ya maradhi kibao

MUME KIGONGO: Damu kwenye mkojo inaweza kuwa dalili ya maradhi kibao

NA LEONARD ONYANGO

UNAPOENDA haja ndogo na kukojoa damu unafaa kuwa na wasiwasi kwani inaweza kuwa dalili ya maradhi hatari.

Magonjwa ya mfumo wa mkojo (UTI) japo hutokea mara nyingi kwa wanawake, wanaume pia wanaweza kuyapata.

UTI hutokea bakteria wanapoingia kwenye mrija unaopitisha mkojo kutoka kwenye kibofu.

Dalili zake ni maumivu ya mgongo, kichefuchefu na kutapika.Kukojoa damu pia kunaweza kuwa dalili ya kujeruhiwa kwa figo, matatizo ya kiafya yanayotokea baada ya kufanya mazoezi magumu kupindukia (Exercise-induced hematuria), kupanuka kwa mfereji wa kupitisha maji ya mbegu za kiume (prostate), kansa ya tezi dume (prostate cancer) na kansa ya kibofu cha mkojo.

Wataalamu wanasema kuwa japo mara nyingi damu kwenye mkojo huwa jambo la kawaida kwa wanaume, ni vyema kuona daktari ili upimwe.

“Mkojo unapopimwa utasaidia kujua kiini cha damu iliyo katika mkojo. Kwa mfano ikiwa mtu anatumia aina fulani ya dawa, anaweza kukojoa damu hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi,” anasema Dkt Angela Makini wa Hospitali ya Penda.

Anasema kuwa wanaume wanaofanya mazoezi magumu kupindukia wanaweza kukoja damu lakini kiini cha hali hiyo hakijulikani.Bakteria wanapoingia kwenye figo kutoka katika damu wanasababisha mwathiriwa kukojoa damu.

“Mkojo kwenye damu unaweza kuwa dalili ya kansa ya figo, tezi dume au kibofu cha mkojo. Waathiriwa wa aina hizi za kansa wanapoanza kukojoa damu ni ishara kwamba kansa imefikia pabaya na inahitaji matibabu ya haraka,” anasema.

You can share this post!

Nazlin Umar amteua naibu mwenye umri wa miaka 26

BENSON MATHEKA: Mfumo wa usimamizi wa basari ubadilishwe...

T L