• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
BENSON MATHEKA: Mfumo wa usimamizi wa basari ubadilishwe kwa manufaa ya wanafunzi

BENSON MATHEKA: Mfumo wa usimamizi wa basari ubadilishwe kwa manufaa ya wanafunzi

NA BENSON MATHEKA

VISA VYA wanafunzi werevu kutoka familia masikini wanaoripoti katika shule za sekondari mikono mitupu wakiwa na kiu ya kuendelea na masomo vinaongezeka.

Visa hivi vinaonyesha kuwa kuna haja ya kubadilisha mifumo yetu ya basari hasa inayosimamiwa na wanasiasa iweze kufaidi wanaolengwa.

Hivi majuzi, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alielezea kusikitishwa kwake na jinsi basari zinazosimamiwa na wanasiasa zinavyotumiwa.

Kwa ujasiri ambao ni kawaida yake, Profesa Magoha alisema kwamba mipango mingi ya basari ukiwemo wa maeneobunge (NG-CDF) imekolewa na ufisadi huku pesa zikifaidi watoto wa matajiri badala ya wale werevu kutoka familia masikini wanaohitaji karo.

Kauli ya Bw Magoha inaweza tu kutoka kwa mtu mwenye ujasiri na mpenda uwazi kwa kuwa kwa miaka mingi, mipango ya basari imekuwa ikitumiwa na wanasiasa kuzawadi washirika wao.

Matokeo yake yamekuwa ni watoto kutoka familia masikini kukosa kujiunga na shule za sekondari. Ikiwa mwanafunzi anayeitwa shule ya kitaifa kwa kupata alama zaidi ya 400 katika mtihani wa darasa la nane hawezi kupata basari kutoka kwa hazina ya NG-CDF ya eneobunge analotoka, basi hakuna haja ya kuwa na mpango huo.

Wazazi wengi kutoka familia masikini wamelalamika jinsi wanavyohangaishwa na wanachama wa kamati za hazina hiyo.

Wakati umefika kwa hazina hiyo kubadilishwa na mfumo badala kuwekwa ili pesa hizo ziweze kunufaisha watoto wanaolengwa.

Walimu wakuu wa shule wanapaswa kushirikishwa kutambua wanaopaswa kunufaika na basari kwa kuwa wanaelewa hali ya kila mwanafunzi wanayefunza. Hii itapunguza ubaguzi na ufisadi uliokolea hazina hiyo.

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: Damu kwenye mkojo inaweza kuwa dalili ya...

LISHE: Granola

T L