• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:27 PM
MUME KIGONGO: Usipolala vizuri mbegu za kiume zitapungua

MUME KIGONGO: Usipolala vizuri mbegu za kiume zitapungua

NA CECIL ODONGO

KUKOSA usingizi wa kutosha kunaweza kusababisha kufifia kwa nguvu za kiume.

Madaktari wanasema kuwa mwanaume anachukuliwa kuwa amepata usingizi wa kutosha usiku iwapo atalala kwa kati ya saa saba na tisa. Hata hivyo, watu wengi huwa hawazingatii muda huo kutokana na aina ya kazi wanazofanya au shughuli nyingine za kutafuta riziki.

Utafiti uliofanyiwa wanaume 2,676 wa zaidi ya umri wa miaka 67 nchini Amerika, ulibaini kuwa wale ambao hukosa usingizi wa kutosha hukumbwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume.

“Utafiti umeonyesha kuwa kukosa usingizi wa kutosha kunapunguza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mwanaume na hilo linachangia kukosekana kwa hamu ya mapenzi na pia ashiki wakati wa tendo la ndoa. Utafiti huo huo unaonyesha pia kupungua kwa mbegu za kiume pia kunasababisha ukosefu wa usingizi,” ilisema ripoti ya utafiti huo.

Ukosefu wa usingizi wa kutosha pia hupunguza kinga mwilini na kusababisha iwe rahisi mwanaume kukumbwa na magonjwa kama shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari na unene.

“Asilimia 20 ya vijana kuna uwezekano mkubwa wamepungukiwa na mbegu za kiume kutokana na shughuli za kutafuta riziki,” akasema Mtaalamu Karen Rowan kutoka Uingereza kwenye jarida linalochapisha habari za afya, LiveScience.

Kwa hivyo, wale ambao hulala chini ya muda wa saa sita utafiti umeonyesha wanaweza kuwatungisha wapenzi wao mimba kwa asilimia 31 huku wale waliolala kwa muda wa saa tisa zaidi wakiwa na asilimia 49.

  • Tags

You can share this post!

Miungano yatishia usalama kwa uvumi

Kasikasi FC, Kisa FC na Melta Kabiriah Youth ndio mabingwa...

T L