• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
MUME KIGONGO: Wanaume wasiokuwa na hamu ya ngono hufa haraka, wasema watafiti

MUME KIGONGO: Wanaume wasiokuwa na hamu ya ngono hufa haraka, wasema watafiti

NA CECIL ODONGO

WANAUME ambao hawana hamu ya ngono hufa haraka, utafiti umebaini.

Watafiti kutoka Chuo cha Yagamata, Japan, waligundua kuwa wanaume ambao hushiriki tendo la ndoa mara kwa mara huishia kuwa na afya imara, hawana tatizo kisaikolojia na huishi kwa muda mrefu.

Wanasema kuwa kushiriki kuna manufaa kama kuimarisha kinga mwilini, kupunguza shinikizo za damu, kupunguaza msongo wa mawazo na hukabili maradhi ya moyo.

Pia, wasiokuwa na hamu ya ngono mara nyingi hujihisi kuwa wana tatizo la kiafya kwa hivyo wao huishi kuwa na wasiwasi mwingi hasa wale ambao wapo katika uhusiano wa kimapenzi.

Wakiathirika sana, hujitenga na watu wengine kwa kuwa hufikiria hali yao huwadhalilisha.

Utafiti huo ulibaini kuwa kati ya mambo ambayo yanasababisha mwanaume akose hamu ya ngono ni uvutaji sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi na pia msongo wa mawazo.

Utafiti huo ulibainisha kuwa mwanaume ambaye hana hamu ya ngono huzama katika mtindo wa maisha ambayo humsababishia msongo wa mawazo na huandamwa na maradhi hatari.

Maradhi hayo kama ugonjwa wa sukari humsababisha mauti yake haraka.

Aidha utafiti huo pia ulihusisha ukosefu wa hamu ya ngono hasa kati ya wanaume ambao wana umri mkubwa, kama unaowaweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa saratani.

Ili kukabiliana na hali hii, watafiti hao walipendekeza kuwa wanaume wanaokosa hamu ya ngono wanastahili kufunguka na kuzungumzia hali yao hasa kwa washauri na watoaji nasaha.

Pia wanastahili kuzungumzia hali yao ndipo washauriwe jinsi ya kujikwamua kutoka hali hiyo.

  • Tags

You can share this post!

DKT FLO: Jino linanikosesha usingizi, nifanye nini nipate...

Shule 10 za kitaifa zavutia watahiniwa 1m

T L