• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
DKT FLO: Jino linanikosesha usingizi, nifanye nini nipate amani?

DKT FLO: Jino linanikosesha usingizi, nifanye nini nipate amani?

Mpendwa Daktari,

Nina jino moja mdomoni lililooza na ambalo limekuwa likinikosesha raha. Nitakabiliana vipi na shida hii?

Mueni, Nairobi

Mpendwa Mariana,

Uozo huathiri sehemu ya juu ya jino na kusababisha mashimo madogo.

Hii hali hutokea polepole baada ya kipindi kirefu kutokana na bakteria mdomoni, masalio ya chakula (hasa sukari na wanga) na kutosafisha mdomo vilivyo.

Ikiwa uozo huu hautatibiwa mapema, hali hii yaweza sababisha mashimo makubwa kujichimba zaidi kwenye sehemu ya ndani ya meno.

Uozo huu husababisha madoa ya kahawia au meusi, mashimo, hisi na maumivu kwenye meno. Aidha, waweza pata maambukizi kupitia sehemu zilizooza na kusababisha usaha kwenye meno.

Maambukizi haya pia huenda yakaenea katika sehemu zingine mwilini. Ili kudhibiti hali hii, tafadhali muone daktari wa meno ili ufanyiwe uchunguzi, na pia meno yaoshwe. Ikiwa kuna uozo, basi utakabiliwa vilivyo na daktari.

Ili kuzuia meno kuoza, piga mswaki vilivyo angaa mara mbili kila siku pindi baada ya kula, kwa kutumia dawa ya meno iliyo na flouride, ondoa vyakula vilivyokwama katikati ya meno kwa kutumia uzi wa Hariri (floss), kunywa maji kwa wingi, jiepushe na vyakula vya sukari na vitafunio, dhibiti mpigo wa moyo, vile vile chakula kurejea mdomoni kutoka tumboni.

  • Tags

You can share this post!

TIBA NA TABIBU: Wengi hawaelezi waajiri wanapotatizika...

MUME KIGONGO: Wanaume wasiokuwa na hamu ya ngono hufa...

T L