• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Muziki: Wakili Angela Ndambuki aling’ara sana na kundi la Tattu

Muziki: Wakili Angela Ndambuki aling’ara sana na kundi la Tattu

NA MAGDALENE WANJA

KATIKA miaka ya 2000 nchini Kenya, kulikuwa na bendi iliyojumuisha akina dada watatu ambao walivutia wengi kwa muziki wao.

Watatu hao walikuwa kwenye kikundi kilichojulikana kama Tattu jina lililosukwa kutokana na idadi yao.

Kikundi hicho kiliundwa na Bi Angela Ndambuki, Angela Mwandada na Debbie Asila, ambao licha ya kusomea taaluma mbalimbali, waliletwa pamoja na muziki.

Hata hivyo, Bi Angela Ndambuki ambaye ni wakili, amekuwa akijihusisha na utungaji na ulinzi wa sheria za kuwalinda wanamuziki.

“Ndoto yangu ya kuwa mwanamuziki ilianza utotoni wakati dadangu alikuwa akinifunza nyimbo ambazo walifunzwa shuleni, na pamoja naye tuliimba nyimbo hizo hadi usiku,” akasema Bi Ndambuki.

Hii ilifuatiwa na utunzi wa nyimbo mbalimbali ambazo alizirekodi baada ya kukamilisha masomo yake.

Mwanamuziki Angela Ndambuki ambaye alikuwa katika kikundi cha Tatuu kilichovuma mwongo mmoja uliopita. PICHA | MAGDALENE WANJA

Mnamo mwaka 2020, Bi Ndambuki alichaguliwa na Shirikisho la Kuangazia Maslahi ya Sekta ya Muziki Duniani la IFPI kuwa Mkurugenzi wa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Nilifurahia sana kwa uteuzi huo ambao ulinifanya mimi kuwa mkurugenzi wa kwanza katika eneo hili, na nilihitajika kushiriki pakubwa katika kubuni sheria za kuendesha sekta ya muziki,” aliongeza Bi Ndambuki.

Mwanzoni mwa mwaka 2023, Bi Ndambuki pia alichaguliwa mwenyekiti wa kwanza wa kike wa Shirika la Wazalishaji wa Muziki Nchini – Kenya Association of Music Producers (KAMP).

Watatu hao wanposherehekea miaka 20 katika sekta ya muziki, wana matumaini ya pengine kujumuika na kufanya muziki pamoja.

  • Tags

You can share this post!

CJ Koome aonya wanaonyemelea na kunajisi watoto

Jambazi wa kuwekea walevi mchele ashtakiwa kwa wizi wa...

T L