• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Njia za asili za kudhibiti shinikizo la damu

Njia za asili za kudhibiti shinikizo la damu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

SHINIKIZO la damu au shinikizo la juu la damu ni hali ya kiafya ya muda mrefu ambapo nguvu ambayo damu inapita katika mishipa yako ni ya juu zaidi ya kiwango cha kawaida kilichobainishwa.

Hufanya moyo kufanya kazi kwa bidii zaidi kusukuma damu dhidi ya shinikizo hili la juu, na kuathiri mishipa ya damu na viungo muhimu kwa muda mrefu.

Shinikizo la damu ni nguvu inayotolewa na mtiririko wa damu dhidi ya kuta za ateri. Kwa watu wazima, kipimo cha kawaida cha shinikizo la damu ni 120/80 mm Hg.

Wakati kwa baadhi ya watu shinikizo la damu hupanda hadi 130/80 mmHg au zaidi. Inaweza kugunduliwa kwa kuangalia shinikizo la damu kwa kutumia chombo cha kupima.

Udhibiti wa shinikizo la damu unahusisha lishe na marekebisho ya mtindo wa maisha pamoja na matibabu yaliyowekwa.

Hapa kuna njia chache za asili za kudhibiti shinikizo la damu ambazo unaweza kujaribu baada ya kuongea na daktari wako.

Marekebisho ya mtindo wa maisha.

Zoezi la kawaida. Chagua shughuli yoyote ya kimwili inayofaa kwako. Unaweza kujaribu kutembea, kukimbia, yoga, kuogelea au Zumba.

Usingizi mzuri. Kulala na kuamka wakati sawa kila siku kuna faida kwa afya yako. Usingizi wa saa 7-8 hchukuliwa kuwa wenye afya.

Kupunguza mawazo. Yoga, kutafakari na kuzingatia ni baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kukusaidia kuzuia matatizo na mkazo unaohusiana nayo.

Kupunguza uzani. Watu walio wanene sana wako kwenye hatari kubwa ya kupata shinikizo la damu na magonjwa ya moyo. Ni muhimu kudumisha uzito wa mwili wako na mzunguko wa kiuno katika safu yenye afya.

Marekebisho ya chakula. Jumuisha matunda na mboga mboga zaidi za msimu katika mlo wako.

Dumisha uwiano mzuri wa wanga bora, nyuzinyuzi, protini na mafuta yenye afya kwenye sahani yako.

Punguza chumvi ya ziada na vyakula vya kukaanga.

Figili. Figili huwa na madini ya potasiamu nyingi, nyuzi lishe, vitamini K, manganisi na kadhalika. Potasiamu ni muhimu kwa moyo na inaweza kusaidia kudhibiti shinikizo la damu.

Shayiri

Uji wa shayiri ni chanzo kikubwa cha nyuzi. Shayiri ni mojawapo ya tiba za asili dhidi ya shinikizo la damu.

Kitunguu saumu

Kitunguu saumu kinajulikana kuwa mojawapo ya tiba bora za nyumbani kwa shinikizo la damu.

  • Tags

You can share this post!

Vidokezo vya maandalizi ya chakula kwa wenye shughuli nyingi

MAPISHI KIKWETU: Pilipili ya kukaanga

T L