• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Vidokezo vya maandalizi ya chakula kwa wenye shughuli nyingi

Vidokezo vya maandalizi ya chakula kwa wenye shughuli nyingi

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MKIWA wazazi, mnataka kuhakikisha kwamba watoto wenu wanakula vizuri na njia bora ya kufanya hivyo ni kuandaa vyakula vinavyopikwa nyumbani mara kwa mara.

Milo iliyopikwa nyumbani hukupa udhibiti zaidi juu ya wingi na ubora wa chakula unacholisha familia yako.

Unaweza kuamua juu ya viungo vya kutumia na aina gani ya chakula. Muhimu zaidi, unakuwa mwangalifu zaidi juu ya kile ambacho familia yako inakula. Kwa ujumla, watu wanaopika na kula vyakula vilivyopikwa nyumbani mara nyingi huwa wamezingatia zaidi lishe bora kuliko wale wanaokula kwingineko.

Ingawa kupika nyumbani kuna manufaa kadhaa, inaweza kuwa vigumu kudumisha, hasa kwa akina mama au hata akina baba wenye shughuli nyingi. Unaposhughulika na kazi yako na kazi nyingine za nyumbani, kuandaa chakula kitamu kilichopikwa nyumbani kwa familia yako kila siku huenda ikakulemea nyakati nyingine.

Lakini ukijipanga vizuri, kuandaa na kupika mlo wenye afya kwa familia yako kunawezekana, hata kwa wenye shughuli nyingi. Hapa kuna vidokezo vya kuandaa chakula akina hata ukiwa na shughuli nyingi.

Andaa menyu yako ya wiki mapema

Mojawapo ya sababu zinazowafanya watu wengine kuchukua muda mrefu kuandaa chakula ni kwa sababu wanaamua tu juu ya mlo wa siku hiyo hiyo. Wanaangalia kiungo chochote kilichosalia kwenye jokofu au kabati la chakula na kupanga chakula chao kutoka hapo. Kwa bahati mbaya, kufanya hivi kutachelewesha tu utayarishaji wako wa chakula hata zaidi.

Kwa hivyo, unashauriwa kuandaa menyu yako ya kila wiki mapema. Kwa mfano, unaweza kupanga kila Ijumaa au Jumapili ya juma kuwa ‘siku yako ya kupanga menyu.’ Katika siku hii, unapitia kabati na friji yako ili kuangalia viungo, matunda, na mboga zilizobaki ulizo nazo. Kutoka huko, unaweza kuamua ni chakula gani au mlo za kupika kwa wiki ijayo. Unaweza pia kuandika viungo ambavyo unakosa ili uweze kuvinunua.

Kuwa na vifurushi vya smoothie vilivyogandishwa

Wakati mwingine, utayarishaji wa chakula huchukua muda mrefu ikiwa bado unahitaji kukata viungo, kama vile matunda au mboga. Kwa hivyo, zingatia kuandaa vifurushi vya smoothie na uvigandishe ili kuokoa muda.

Unaweza kuandaa haraka na kujumuisha matunda na mboga mboga katika milo ya kila wiki ya familia yako bila kuhitaji kukata vipande vipande.

Tumia vyombo vya chakula vya ubora wa juu

Unaweza kuwa unashangaa jinsi vyombo vya chakula vinavyoweza kusaidia kupunguza utayarishaji wako wa chakula. Lakini ikiwa umegundua, wakati huna vyombo vya chakula, huwa unatumia muda mwingi kufungua viungo vilivyopakiwa na kujaribu kuvirudisha. Unapokuwa na haraka au una shughuli nyingi sana, huenda usiweze kuviweka katika nafasi nzuri, na kuacha jikoni yako ikiwa bila mpangilio.

Kwa utayarishaji wa chakula nadhifu na kwa njia ya haraka zaidi, unaweza kuwekeza katika vyombo vya ubora wa juu ambapo unaweza kuhifadhi viungo vyako vyote, ikiwa ni pamoja na mabaki yako.

Ikiwezekana, chagua vile vilivyotengenezwa kwa glasi au plastiki, ambapo unaweza kuona kile kilichohifadhiwa ndani. Kwa hivyo, unapovihitaji wakati unaandaa chakula, unaweza kugundua kwa urahisi chombo gani cha kuvuta na kutumia kwa utayarishaji wako wa chakula. Zaidi ya hayo, kutumia vyombo vya ubora wa juu vya chakula kunaweza kufanya chakula chako kiwe safi na kufanya mabaki yako yaonekane ya kuvutia zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Watengenezaji malisho ya mifugo waomba muda kuongezwa...

Njia za asili za kudhibiti shinikizo la damu

T L