• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Pilipili ya kukaanga

MAPISHI KIKWETU: Pilipili ya kukaanga

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 15

Inatengeneza kopo moja

Vinavyohitajika

  • vitunguu maji 2
  • punje 4 za kitunguu saumu
  • tangawizi
  • pilipili 15 zilizokatwa
  • nyanya 2
  • kijiko 1 ½ cha nyanya ya kopo
  • kijiko ½ cha paprika
  • kijiko ½  cha manjano
  • kijiko ¼ cha bizari nyembamba
  • karoti 1 iliyokatwa
  • juisi ya limau kijiko ½
  • kijiko 1 cha sukari ya kahawia

Maelekezo

Unaweza kutumia aina nyingine yoyote ya pilipili, hata hivyo pilipili mbichi hakika ni bora zaidi.

Kwenye sufuria yako iliyo na mafuta na chumvi, weka vitunguu vyekundu, pilipili mbichi zilizokatwakatwa, tangawizi na kitunguu saumu.

Kaanga mpaka vilainike na viwe na harufu nzuri. Aidha, kitunguu saumu na tangawizi ikiwa ni sehemu ya viungo vya pilipili ya kukaanga huongeza ladha zaidi.

Ongeza nyanya, nyanya ya kopo na viungo. Viungo lazima vichemke vizuri hivyo usiharakishe mchakato.

Ongeza kikombe robo cha maji ya moto.

Mara tu nyanya zikiiva kabisa na viungo vimeyeyuka, baada ya kama dakika 10, ongeza karoti zilizoparwa, sukari ya kahawia na maji ya limau.

Ongeza kikombe robo cha maji ya moto na acha kitoweo hiki kiive kwenye moto wa wastani hadi chakula kiwe kizuri na kizito.

Acha chakula kiive kwa dakika kama 10.

Epua na chakula kikishapoa, weka kwenye kopo tayari kutumia.

  • Tags

You can share this post!

Njia za asili za kudhibiti shinikizo la damu

Faida za kuwa na kijishamba cha mboga nyumbani

T L