• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Njia rahisi za kufuta madoa meusi kwenye kisugudi na goti

Njia rahisi za kufuta madoa meusi kwenye kisugudi na goti

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MARA nyingi ngozi nyeusi kwenye kisugudi cha mkono na hata kwenye goti husababishwa na mkusanyiko wa seli zilizokufa kutokana na msuguano kwenye sehemu hizo.

Kwa kawaida, sehemu hizi huwa kavu na hazina uwezo wa kutoa mafuta kama sehemu nyingine za ngozi na hivyo zinahitaji kutunzwa na kufanywa kuwa safi.

Ukiwa na mzoea ya kuweka kisugudi chako kwenya meza wakati unafanya kazi ama kukutanisha goti lako na kisugudi wakati ukifua au kwenye shughuli shambani, ule msuguano hufanya ngozi yako katika maeneo hayo iwe nyeusi.

Tango

Kama ilivyo kwa ndimu, imethibitishwa tango nalo lina uwezo mkubwa katika kuifanya ngozi kuwa nyeupe. Lina uwezo mkubwa wa kuzuia ngozi kuharibika na lina vitamini A na C ambazo ni muhimu sana katika kuiboresha ngozi na kuifanya iwe laini tena.

Kwenye mchanganyiko wako unaweza kuongeza juisi ya limau kabla ya kuupaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

Ndimu na magadi

Ndimu imethibitishwa kuwa kiungo muhimu katika kuifanya ngozi kuwa nyeupe. Ina uwezo mkubwa wa kuzuia ngozi kuharibika na vitamini C ambavyo ni muhimu sana katika kuiboresha ngozi na kuifanya iwe laini tena. Kwa kutumia pamba, kitambaa safi au tunda lenyewe tu, paka juisi ya ndimu iliyochanganyika na magadi kiasi katika sehemu zenye weusi. Tulia nayo kwa muda wa saa moja kisha osha sehemu hiyo. Rudia kila siku hadi weusi utakapopotea.

Mshubiri na maziwa

Unachotakiwa kufanya ni kupaka mchanganyiko wako kwenye sehemu yenye uweusi na uache kwa nusu saa hivi au hata usiku mzima na ioshe sehemu hiyo kwa maji ya ufufutende kabla ya kuipaka mafuta ya kulainisha. Rudia kufanya hivi mara mbili kila siku hadi utakapoona matokeo bora zaidi.

Mshubiri. PICHA | MARGARET MAINA

Viazi mviringo

Kiazi kina kimeng’enya ambacho kinasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa uweusi kwenye ngozi bila ya kuongeza chochote.

Ukikikata na kukipaka kwenye ngozi yako hasa maeneo ya kisugudi na goti kwa dakika 15 hivi kabla ya kuosha kwa kutumia maji ya ufufutende, na kurudia kwa siku kadhaa, basi utaona ngozi yako ikianza kuwa nyororo na pia mabaka meusi yakipotea.

Sukari na mafuta ya zaituni

Mchanganyiko wa sukari na mafuta ya zaituni utakusaidia kuimarisha ngozi yako na hata kuondoa seli zilizokufa kwenye magoti na mikono. Paka mchanganyiko wako katika sehemu zenye uweusi kisha sugua kwa utaratibu na polepole kama unakanda hivi. Kisha osha maeneo hayo kwa maji ya ufufutende kabla ya kuyakausha na kupaka mafuta ya kulainisha. Rudia mara kadhaa kwa wiki au muda zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Michirizi mwilini na namna ya kuiondoa

ULIMBWENDE: Matumizi ya ukwaju ni mengi

T L