• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
ULIMBWENDE: Matumizi ya ukwaju ni mengi

ULIMBWENDE: Matumizi ya ukwaju ni mengi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

WENGI wetu huwa tunakula ukwaju moja kwa moja lakini wako wanaopenda kutengenezea sharubati, wengine ice cream, na baadhi kuweka katika chakula kama kinogesho na kadhalika.

Lakini tunda hili pia hutumika kutengeneza bidhaa za urembo ikiwemo sabuni.

Je, tunda hili la ukwaju lina faida gani katika urembo?

Hutibu madhara yanayotokana na vipodozi vya kemikali

Wengi tunatumia vipodozi vikali ili kubadilisha ngozi zetu kuwa nyeupe bila ya kufahamu kuwa vipodozi hivyo vina kemikali ya hydroquinone.

Hydroquinone inasababisha kansa kwa kuuwa melanin (chembechembe za rangi kwenye ngozi). Mbali na kansa, aina hizo za sabuni na vipodozi vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha mwili kutoka mabaka na michirizi.

Ngozi kuwasha na kuvimba

Sabuni ya asilia iliyotengenezwa kwa ukwaju inaweza kuondoa madhara hayo ndani ya muda mfupi.

Hutakatisha ngozi yako

Tunda la ukwaju lina AHA (Alfa Hydroxy Acid) ambayo husafisha ngozi kwa kuondoa seli zilizokufa na kuacha ngozi ambayo ni mpya lakini pia husaidia kuondoa na hufungua vitundu vya vinyweleo na kuondoa makunyanzi yatokanayo na umri kuenda.

Hupunguza makunyanzi usoni

Kwa msaada wa vitamin B na AHA zilizopo ndani ya tunda la ukwaju, hufungua vitundu vya hewa kwenye ngozi na kuruhusu mpishano mzuri wa hewa hivyo ngozi huwa na unyevu masaa yote na kusababisha makunyanzi kutoweka.

Husawazisha ngozi inayopona baada ya kuungua au ile yenye kidonda

Kiungo cha AHA kinasaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa, kitu ambacho husaidia kuondoa makovu mwilini yaliyosabaishwa na vidonda, matumizi ya vipodozi vyenye kemikali kali au kuungua kwa moto.

Huondoa chunusi na harara

Tunda la ukwaju limo katika orodha ya matunda yaitwavyo “Anti Inflammatory Fruits“ yenye sifa ya kuponya vidonda. Ukwaju huwa na asidi ambayo hufyonza mafuta ya ziada katika ngozi. Hii husaidia kuzuia chunusi katika ngozi. Kama tujuavyo chunusi hutokana na mrundikano wa mafuta yasiyo na kazi katika ngozi.

Hutibu uvimbe unaotokea mtu anapoumwa na wadudu

Kwa vile tunda la ukwaju lina sifa ya kuwa ni ‘Anti-Inflammatory’, basi lina uwezo wa kufyonza sumu iliyoachwa na mdudu baada ya kukuuma.

Hung’arisha na kulainisha ngozi kwa muda mfupi sana

Kwa vile ukwaju una kirutubisho cha AHA, chembechembe za ngozi zilizokufa na uchafu huondolewa haraka. Ngozi inabaki ikiwa laini na ya kung’ara.

Husaidia kuzibua matundu ya jasho na kuifanya ngozi iwe na unyevu siku nzima

Matundu ya jasho yanaruhusu jasho kutiririka kutoka mwilini endapo joto la mwili litazidi. Ikiwa matundu hayo yatazibika, bakteria watakusanyika na kusababisha chunusi na uvimbe. AHA ndani ya ukwaju husaidia kuzibua matundu hayo na kuruhusu jasho kutoka bila ya matatizo yoyote.

You can share this post!

Njia rahisi za kufuta madoa meusi kwenye kisugudi na goti

Mke wa mkosoaji wa Museveni ashtaki polisi

T L