• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Pigo kwa Mandonga Mtu Kazi bodi ikimzaba marufuku ya kushiriki ndondi

Pigo kwa Mandonga Mtu Kazi bodi ikimzaba marufuku ya kushiriki ndondi

NA SAMMY WAWERU

MWANABONDIA hodari wa Tanzania, Karim Mandonga maarufu kama Mtu Kazi amepata pigo baada ya Bodi Kutathmini Ndondi Nchini humo (TPBRC) kumzuia kwa muda kushiriki mapigano.

Duru zinaarifu, taasisi hiyo imetoa uamuzi huo hadi pale atakapofanyiwa uchunguzi kubaini “ufaafu wake kiafya”.

Kulingana na TPBRC, Mandonga ataruhusiwa kushiriki ndondi endapo atathibitishwa kuwa sawa kimawazo-kiakili na kimwili.

Shirika la Habari la ZBC, Zanzibar liliripoti Jumanne, Agosti 15, 2023 kuwa bodi husika ilitoa marufuku hiyo kutokana na hofu ya usalama wake kiafya.

“Karim Mandonga ataruhusiwa kurejea kuporomosha mangumi ikithibitishwa kuwa ni salama kiafya,” runinga hiyo ikaarifu.

Aidha, ukaguzi huo utanyika katika Hospitali ya Kitaifa ya Muhimbili.

Mandonga, aligonga vichwa vya habari Julai 2023 baada ya kuangushiwa mangumi mazito na kushindwa na mwanabondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi katika mapigano jijini Nairobi, licha ya majivuno na umaarufu wake katika ndondi.

Mwezi huu, Agosti, mwanandondi huyo tena alilimiwa nyumbani – Tanzania na mwanabondia Moses Golola wa Uganda.

Akijitambua kama mwanabondia hodari Afrika Mashariki, alidai kichapo alichoangushiwa na Golola huenda alifanyiwa uganga ama mazingaombwe.

Tangazo la marufuku ya Mandonga, hata hivyo, limeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki wake mitandaoni baadhi wakikosoa tangazo la TPBRC.

  • Tags

You can share this post!

Barabara za lami mpya zafanya Industrial Area kung’aa

Mwangaza ajipata gizani akitakiwa kuwajibikia Sh42.4 milioni

T L