• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Raila: Sauti ya Kindiki ni dhaifu sana kumtambua

Raila: Sauti ya Kindiki ni dhaifu sana kumtambua

NA SAMMY WAWERU

RAILA Odinga, kiongozi wa Azimio, anaendelea kuendesha mashambulizi yake kwa Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki, akidai kuwa sauti yake ni dhaifu sana kwake kumtambua kama bosi wa masuala ya usalama nchini.

Akizungumza na wakazi wa Emali katika Kaunti ya Makueni mnamo Jumanne, Agosti 15, 2023, kiongozi huyo wa upinzani kwa utani alidai kwamba hawezi kutofautisha sauti ya Prof Kithure na ile ya mwanamke.

“Kuna huyu mtu, sijui ni Gachagua ama Kindiki, anayepiga kelele nyingi zisizosikika. Siwezi kubaini ikiwa yeye ni mwanaume au mwanamke,” alieleza.

Kiongozi huyo wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) amekuwa akizozana na Waziri Kindiki na Naibu Rais, Rigathi Gachagua.

Waziri Mkuu huyo wa zamani aliambia wakazi wa Emali kuwa, upinzani hautayumbishwa na vitisho vya Prof Kindiki kuhusiana na maandamano ya Azimio la Umoja.

“Anatutishia endapo tutaamua kurudi barabarani kuandamana…Tutaaendelea. Sisi ni Wakenya, na hatutajisalimisha kwa vitisho vyao,” Bw Odinga alisisitiza.

Licha ya kusitishwa kwa maandamano ya Azimio kwa ajili ya kuomboleza wafuasi waliopoteza maisha kutokana na ukatili wa polisi, pamoja na kufanikisha mazungumzo kati ya upinzani na serikali ya Kenya Kwanza, Odinga anasisitiza kwamba lengo lake ni kuona gharama ya maisha inashuka.

Azimio pia inataka sava ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kufunguliwa, ili kubaini ukweli wa matokeo ya urais ili uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

“Tumeweka wazi kuwa gharama ya maisha lazima ishushwe, na sava ya IEBC ifunguliwe.”

 

  • Tags

You can share this post!

Raila adai Cherera na Masit wako mafichoni

Mkenya avunja rekodi ya mpishi kutoka Amerika

T L