• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Sabina Chege: Yaliyopita si ndwele

Sabina Chege: Yaliyopita si ndwele

Na SAMMY WAWERU

SIKU moja baada ya kupewa marufuku ya muda bungeni, mbunge maalum Sabina Chege amehimiza haja ya kusahau yaliyopita.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, Bi Sabina ameelezea Ijumaa, Juni 9, 2023 umuhimu wa ‘kuachilia ya jana – yaliyopita’.

“Achilia ya jana yapite. Leo iwe mwanzo mpya na ufanye bora, Mungu atakufanikisha ufike unapolenga,” mbunge huyo akaandika.

Alhamisi, Juni 8, mvutano bungeni ulizuka kati ya wabunge wa upinzani, Azimio la Umoja-One Kenya na wa mrengo tawala wa Kenya Kwanza, Azimio ikishinikiza Bi Sabina avuliwe wadhifa wa naibu kiranja wa wachache bungeni.

Kundi la Azimio limekuwa likitaka mbunge mwakilishi huyo wa wanawake wa zamani Murang’a ajiuzulu, kwa kutokuwa ‘mwaminifu chamani’.

Licha ya kuteuliwa bungeni kupitia Jubilee, anaunga mkono serikali ya Rais William Ruto.

Jubilee ni mojawapo ya vyama tanzu vinavyounda muungano wa Azimio, unaaongozwa na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga.

Wakati wa uchaguzi mkuu 2022, Sabina alikuwa anapigia debe Bw Odinga kuingia IKulu.

Wabunge 7, akiwemo Bi Sabina walipewa marufuku ya majuma mawili bungeni na wengine siku tano.

Spika Moses Wetangula, alisema hawezi kumvua wadhifa wake, naibu kiranja wa wachache bungeni, akihoji mikono yake imefungwa na amri ya korti kuzuia Sabina asifurushwe.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Amadi apata afueni mahakama ikiagiza akaunti zake za benki...

Mwanamume arudi nyumbani kwa likizo na kupata madume...

T L