• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Shari Afrika awaza kubeba tuzo ya Grammys

Shari Afrika awaza kubeba tuzo ya Grammys

Na JOHN KIMWERE

PENYE nia pana njia. Ndivyo wahenga walivyologa, tangia zama zile baada ya kupasua hilo mpaka sasa, msemo huo ungali na mashiko siyo haba miongoni mwa jamii kwa jumla.

Sharon Achieng Winnie maarufu Shari Afrika ni alianza kughani nyimbo zake kimzaha akiwa kidato cha kwanza. Binti huyu anasema ndani ya miaka mitano ijayo amepania kuwa kati ya wasanii wanaopeperusha bendera ya Afrika na kutwaa tuzo ya Grammys.

Aidha ndani ya kipindi hicho anataka kuwa amefanikiwa kuachia album tano na kuzuru zaidi ya mataifa kumi akitumbuiza wapenzi wa nyimbo za burudani. Msupa huyu amehitimu kwa shahada ya digrii kwa masuala ya mipango na menejimenti katika chuo kikuu cha Moi.

Kando kuwa msanii dada huyu ni meneja katika kampuni ya Darasa pia hutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa mbali mbali (Influencer Marketer) kwenye kampuni ya LG.

”Nilianza bila kutarajia lakini kiukweli ninapenda kufanya kazi ya muziki umenifungulia milango kwa kiwango ambacho sikutarajia,” anasema na kuongeza kuwa anaamini atatimiza ndoto yake. Alizamia uimbaji akiwa shule ya msingi alipojiunga bendi ambapo walikuwa akiimba nyimbo za Rhumba, Lingala na Folk Fusion.

Sharon Achieng Winnie maarufu Shari Afrika…Picha/JOHN KIMWERE

Enzi hizo alipenda kusikiza nyimbo zake Vybz Kartel mzawa Jamaica. Katika mpango mzima alenga kutinga upeo wa msanii Ayub Oganda aliyeibuka bila kutarajiwa.

Dada huyu anatunga nyimbo za mitindo ya Folk Fusion na Pop-Folk. Anasema anaamini ipo siku muziki wake utakubalika na kutinga kiwango cha kujaza stadium nzima kama mwana dada anayekuja kwa kasi, Zuchu mwimbaji wa bongo fleva. Amefanikiwa kuachia nyimbo nyingi ikiwamo ‘Ng’inya,’ ‘Dala,’ na ‘Msanii.

Mwaka huu akishirikiana na wasanii wengine wameachia vibao kama ‘Serereka’ na ‘Vumulia’ zote akishirikiana na Trio Mio.Kwa jumla anasema amefanya nyimbo nyingi na wasanii kama Trio Mio, Ngalah Oreyo, Max Doblhoff, Village Cuts, Darwin, Yaba, Noble Afrika na Tayllor kati ya wengine. Anasema anaendelea kuweka mipango sawa na wasanii wengine wanaopania kufanya muziki nao.

Pia amerekodi kibao kiitwacho ‘Pesa’ kilichodhaminiwa na Goethe Institute na Boxhouse Music. Aidha ameachia ‘Nyaboma’ kazi iliyofanywa na produsa Max Doblhoff raia wa Australia. ”Fataki hii inazungumzia jinsi watu wa mashambani nyakati zingine hawaelewi mienendo ya wakazi wa mijini,” akasema.

Kwa sasa yupo jikoni anandaa nyimbo mpya kwa kichwa ‘Fanyanga’ anayosema anaamini kuwa itabamba. Humu nchini angependa kufanya kazi nao Suzanna Owiyo bila kuweka katika kaburi la sahau Sanaipei Tande ambao wameghani teke kama Wamiel na Amina mtawalia.

Duniani angependa kufanya kazi kibao nao Ruby mtunzi wa Bongo Fleva ambaye amefanya kazi kama ‘Alele, na ‘Na yule,’ kati ya zingine. Pia anataja kuwa furaha endapo itapata fursa kutua jukwaa moja na msanii mzawa wa Nigeria Simisola Bolatito Kosoko maarufu Simi.

Msanii huyu anajivunia kutunga fataki kama Smile for me, Women na ‘Loving’ kati ya zingine. Dada huyu anajivunia kutwaa tuzo ya The Headies award for the album of the Year.

 

You can share this post!

Caroline ajivunia kuwa mwingizaji

Kivumbi kushushwa fainali KJ Super Cup

T L