• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Siri kuokoa nyanya zinazopotelea shambani na kwenye masoko

Siri kuokoa nyanya zinazopotelea shambani na kwenye masoko

NA SAMMY WAWERU

REUBEN Muriithi amekuwa mkulima wa nyanya kwa zaidi ya miaka minane na huzalisha kiungo hicho cha mapishi eneo tambarare na kwenye kivungulio.

Alianza kilimo cha nyanya kiungani mwa jiji la Nairobi kabla kuhamia eneo la Meru anakokiendelezea.

Sawa na wakulima wengine, Muriithi amekuwa akipitia changamoto za soko hasa kwa sababu ya masoko mengi nchini ya mazao mabichi ya shambani kuvamiwa na mabroka.

Mawakala wanawapunja wakivuta ngoma upande wao, wakiridhia mapato ya jukwaa ambalo hawakushiriki kuandaa.

Maji huzidi unga mavuno yanapofurika sokoni, mengi yanaishia kuharibika na kuoza.

“Kwa anayekosa kuwa mateka wao, mazao yake yanaozea shambani,” mkulima Muriithi aelezea.

Malalamiko yake si tofauti na ya Erastus Muriuki, mkulima wa nyanya Kaunti ya Kirinyaga.

“Mwaka wa 2005 nilikuwa nakuza nyanya hadi zaidi ya ekari 20, kwa sasa ninalima chini ya ekari 10,” Muriuki adokeza, akilalamikia kero ya mawakala.

“Awali, kreti cha nyanya kilikuwa cha kilo 60. Mabroka sasa wanapakia hadi kilo 130, ni hujuma kwa wakulima.”

Ni mahangaiko ya kilimo-biashara yanayomhuzunisha Betsy Gonnah ambaye ni mjasirimali anayeongeza thamani mazao mabichi ya shambani.

“Inasikitisha kuona nyanya zikiharibika na kuozea kwenye mashamba na sokoni, ilhali zinaweza kuongezwa thamani,” Betsy aelezea.

Akiwa mwenyeji wa Kitengela, Kaunti ya Kajiado, Betsy na mume wake hutengeneza sauce na paste kwa kutumia pilipili kichaa na nyanya.

Betsy Gonnah katika maonyesho ya nyama, Nairobi KICC Meat Expo mwishoni mwa mwaka uliopita, akielezea anavyotengeneza bidhaa kwa kutumia mazao ya shambani. PICHA | SAMMY WAWERU

Alipata ujuzi na maarifa hayo kupitia Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Nchini (KIRDI).

“Niliingilia uundaji wa chilli na tomato paste na sauce baada ya Kenya kukumbwa na janga la Covid-19,” adokeza.

Mfanyabiashara huyu mwenye kandarasi na baadhi ya wakulima wa pilipili na nyanya kumsambazia bidhaa, hutumia mashine ya kusaga (pulper), kupasha joto (pasteurizer), kuchemsha na kusaga ikichanganya (blender), na pia kipimajoto, kuendeleza shughuli hiyo.

Vilevile, hutumia maabara ya KIRDI yenye makao yake makuu South C, Nairobi.

Viungio anavyotumia ni vitunguu vyekundu vya mviringo, karoti, maembe, vitunguu saumu na celery.

“Hujiri na muundo wa sauce na paste,” Betsy aelezea.

Hutoa maganda ya mazao, kisha yanapitia taratibu za kupata juisi na mengine kusagwa, anachanganya na viungio, halafu anapika.

KIRDI imemnoa bongo kiasi cha kuelewa bayana kujiri na bidhaa anazotengeneza na kupakia.

“Kuongeza mazao mabichi thamani si kazi ngumu, vifaa vingi vinavyotumika ni vilivyoko majikoni mwetu. Ni muhimu pia kupata ujuzi maalum kupitia KIRDI.”

Huku wakulima na wafanyabiashara sokoni wakiendelea kukadiria hasara mazao yanapokosa kununuliwa kuisha, Betsy anahisi uongezaji thamani utawaletea suluhu.

Miongoni mwa Ajenda Nne Kuu za Rais Uhuru Kenyatta kabla kustaafu mwaka huu, ni kuboresha sekta ya viwanda.

Aidha, kulingana na Betsy kiini cha kuwa na viwanda dhabiti ni kufanikisha sekta ya kilimo, akipendekeza mazao kuongezwa thamani.

Ni muhimu kukumbusha kiongozi wa nchi kwamba bidhaa zilizoongezwa thamani zinavutia soko ndani na nje ya nchi, bei nayo ikiwa bora zaidi.

Takwimu za Faitrade Africa, shirika linalotafutia wakulima soko kimataifa zinaonyesha mazao yaliyoongezwa thamani yana ushindani mkali.

  • Tags

You can share this post!

Miili ya wavulana watatu yapatikana kwenye kidimbwi Juja

KAULI YA MATUNDURA: Waandishi watatu wa Zanzibar...

T L