• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 12:41 PM
Staa wa TV aomba msaada baada ya kulemewa na dawa za kulevya   

Staa wa TV aomba msaada baada ya kulemewa na dawa za kulevya  

NA MERCY KOSKEI

ALIYEKUA mwanahabari wa runinga ya Citizen, Kimani Mbugua ametoa wito kwa Wakenya kumsaidia ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Kupitia kwa akaunti yake ya Instagram, Bw Kimani alichapisha video mnamo Jumamosi Septemba 23, 2023 akiomba msaada akifichua kuwa kwa sasa hana makao.

Kimani Mbugua alidokeza kwamba alipoteza makao baada ya watu waliomsitiri awali kumtaka asirejee, hivyo kumlazimu kuomba usaidizi kutoka kwa mashabiki wake mitandaoni na wasamaria wema.

“Habari zenu, Kimani Mbugua hapa nyota wa zamani wa TV. Naskia vibaya nikisema hivyo sasa kwa sababu mimi si staa tena. Lakini niko kwa shida, na ninahitaji msaada wenu,” Kimani alisema kupitia video hiyo

“Kama ningekuwa nimekufa, watu wangekua wanasema ooh Kimani alikuwa hivi ama hivo. Sitakubali kuteseka. Kwa upande mwingine, sitaki kuonyesha kama nachangiwa pesa ya kufanya kitu kibaya,” aliongeza.

Mtangazaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 27, alisimulia mapambano yake na ugonjwa wa akili na matumizi ya dawa dawa za kulevya.

Kulingana naye, kwa muda wa wiki moja baada ya kutoka hospitalini, amebuni mpango wa biashara na kwamba anahitaji tu mshirika wa kusaidia ufadhili.

“Nilitoka hospitalini wiki iliyopita na ninahisi akili yangu imerejea katika hali ya kawaida. Sitaki kurejea mahali nilipokuwa zamani,” alisema.

Alibainisha kuwa aliazima simu ambayo aliitumia kuchukua video hiyo akiomba msaada na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii ili apate usaidizi.

“Ukitaka kunisaidia, barua pepe yangu ni [email protected],” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Ulijua sumu ya nyuki inatibu Athritis?

FATAKI: Wakati umewadia tuongee kuhusu visa vya mauaji ya...

T L