• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
FATAKI: Wakati umewadia tuongee kuhusu visa vya mauaji ya kinyama hasa kati ya jinsia hizi mbili

FATAKI: Wakati umewadia tuongee kuhusu visa vya mauaji ya kinyama hasa kati ya jinsia hizi mbili

NA PAULINE ONGAJI

KUNA kisa ambacho kimekuwa kikigonga vichwa vya habari, ambapo kaka mmoja (Mungu ailaze roho yake mahali pema) aliuawa kinyama kwa kudungwa kisu mara kadhaa.

Tukio hilo liliwaacha wengi vinywa wazi huku baadhi ya watu wakijiuliza nini hasa kinachoweza mchochea binadamu kuingiwa na ghadhabu ya aina hiyo, kiwango cha kumtendea mwenzake unyama wa aina hiyo.

Jibu ni kwamba dunia imejaa watu walio na kichaa ambao kwa kiwango fulani kimechochewa na mkusanyiko wa hasira kutokana na matendo maovu wanayokumbana nayo.

Kwanza kabisa sisemi kwamba hiki ndicho kilikuwa kichocheo kwenye kisa hiki, lakini utakubaliana nami kwamba pengine wakati umewadia wa kuzungumzia masuala ya mauaji ya kinyama humu nchini hasa baina ya watu wa jinsia tofauti.

Katika jamii ya sasa, imekuwa kawaida kwa watu kuwatendea wenzao maovu, na kuendelea na maisha yao ya kawaida hata bila kuomba msamaha, pasipo kujali athari walizosababisha.

Kwa mfano, katika masuala ya mahaba, imekuwa kawaida kwa baadhi ya wanaume kuchezea hisia za mabinti na kutoweka.

Dume linamtongoza binti wa wenyewe, kulala naye, kisha kwenda zake bila kujali hisia zake.

Kinachoshangaza ni kwamba, hata kunao wanaosifu tabia hii. Kunao wanaochumbia mabinti kadhaa mara moja na hata hawafichi.

Kaka yuko na binti fulani mahali, ilhali anatumiana jumbe za mapenzi hadharani na mwingine.

Kuna wanaume ambao licha ya kuwa wameoa au wako katika mahusiano, simu zao zimejaa picha za uchi za wapenzi wao wa kando, na hawajali nini chaweza tokea endapo mke au mchumba atakumbana nazo.

Kunao ambao licha ya kuwa wameoa, hata wanawaleta wapenzi wao wa pembeni nyumbani kwao hata mke akiwepo.

Kwa upande wa akina dada, imekuwa kawaida kuzungumzia ule msemo wa kula nauli ya wanaume.

Wanawake wanatafuna senti za akina kaka bila huruma huku wakiwaahidi penzi, ila kutoweka pindi baada ya kunufaika.

Wanawake wanaosomeshwa na wanaume vyuoni huku wakiahidi ndoa, lakini pindi baada ya kukamilisha masomo, wanachana mbuga hata bila asante, huku wakiwaacha wenzao na madeni.

  • Tags

You can share this post!

Staa wa TV aomba msaada baada ya kulemewa na dawa za...

Eliud Kipchoge: Kuibuka mshindi wa Berlin Marathon mara...

T L