• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
TAARIFA ZA WIKI: Kumbatieni lishe ya wadudu kupambana na makali ya njaa, wataalamu washauri

TAARIFA ZA WIKI: Kumbatieni lishe ya wadudu kupambana na makali ya njaa, wataalamu washauri

NA LEONARD ONYANGO

WATAALAMU wamewataka Wakenya kukumbatia lishe ya wadudu kama njia mojawapo ya kukabiliana na makali ya njaa.

Dkt Saliou Niassy wa Taasisi ya Kimataifa ya Kutafiti Wadudu (Icipe) anasema kuwa wadudu wamesheheni virutubisho tele vinavyohitajika kwa afya.

Anasema kuwa mafuta ‘yaliyokamuliwa’ kutoka kwa nzige na nyenje (bush-cricket) katika kituo cha Icipe, yalipatikana na kiwango kikubwa cha mafuta ya omega-3na vitamin E kuliko kiwango ambacho hupatikana kwenye mimea.

Utafiti uliofanywa na Icipe umebaini kuwa zaidi ya aina 500 za wadudu wanaweza kuliwa bila kudhuru afya.

  • Tags

You can share this post!

Maskwota wa Mavoloni wataka usaidizi kutoka kwa serikali

Lamu: Wachuuzi kurudishwa ndani katika soko la manispaa...

T L