• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
TIBA NA TABIBU: Glasi nane za maji kila siku zitakuongezea siku – watafiti

TIBA NA TABIBU: Glasi nane za maji kila siku zitakuongezea siku – watafiti

NA WANGU KANURI

WATU wanaokunywa glasi nane za maji kila siku huishi kwa miaka mingi huku ikiwa nadra kuugua.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Amerika, maji mengi husaidia pia kupunguza magonjwa kama kiharusi au yale ya moyo.

Watafiti hao waliwachunguza watu 11,000 wenye umri wa zaidi ya miaka 30 walichunguzwa viwango vyao vya madini ya sodiamu kwenye damu.

Watafiti hao waligundua kuwa wale ambao sodiamu ilikuwa kwa viwango vya juu, asilimia 64, walikuwa kwenye hatari ya kufariki mapema.

“Kuwa na maji ya kutosha mwilini humuongezea mtu miaka 15 huku kutokuwa na viwango ya kutosha kukifanya mtu kuzeeka kwa haraka kwa kuathirika kwa DNA.”

Wataalamu hao walishauri kuwa ili kuongezea viwango vya maji mwilini, mtu anafaa kunywa maji, juisi, mboga au matunda yaliyo na maji mengi.

Kutokuwa na maji ya kutosha mwilini humfanya mtu kuhisi kizunguzungu, uchovu na kuumwa na kichwa.

  • Tags

You can share this post!

Uhaba wa nafasi kulazimu wanafunzi elfu 24 Pwani kusomea...

TIBA NA TABIBU: Wengi hawaelezi waajiri wanapotatizika...

T L