• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
TIBA NA TABIBU: Wengi hawaelezi waajiri wanapotatizika kiakili

TIBA NA TABIBU: Wengi hawaelezi waajiri wanapotatizika kiakili

NA WANGU KANURI

MFANYIKAZI mmoja kati ya kumi humfahamisha mwajiri wake anapougua maradhi ya akili, utafiti umeonyesha.

Wanasayansi wanaeleza kuwa mfanyikazi mmoja kati ya wanne hulaumu uchovu wa mwili ilhali ni afya yao ya akili ambayo huwa imedorora huku mmoja kwa watano wakienda mapumzikoni kujifurahisha badala ya kutafuta matibabu.

Cha kusikitisha ni kwamba wale walio na umri wa chini ya miaka 24 wapo kwenye hatari maradufu ya kuugua magonjwa ya akili ikilinganishwa na waliozidi umri huo.

Hii ni kwa sababu, wengi wa watu hao hawapendelei kutangamana na wenzao huku wakijitwika kwenye simu zao. Hii huwafanya wengi wao kutozungumzia wanachopitia maishani kwa kujitenga.

Hali kadhalika, ili kuhakikisha kuwa afya ya akili ya wafanyikazi imeimarika, wataalamu hao wamewapendekezea waajiri kufanya juhudi spesheli za kuipa afya ya akili ya waajiriwa wao kipaumbele.

Kampuni nyingi zikiwa na mikakati ya kuhakikisha afya ya kimwili ya wafanyikazi wao iko sawa, wagonjwa wa afya ya akili huhofia kuwaeleza wakubwa wao kwa kuogopa unyanyapaa au hata kupigwa kalamu.

“Cha msingi ni kuhakikisha kuwa wafanyikazi wanaweza kuzungumzia mambo wanayopitia bila hofu,” wanasema wataalam hao.

  • Tags

You can share this post!

TIBA NA TABIBU: Glasi nane za maji kila siku zitakuongezea...

DKT FLO: Jino linanikosesha usingizi, nifanye nini nipate...

T L