• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 7:50 AM
Uhaba wa nafasi kulazimu wanafunzi elfu 24 Pwani kusomea bara

Uhaba wa nafasi kulazimu wanafunzi elfu 24 Pwani kusomea bara

NA LEONARD ONYANGO

ZAIDI ya wanafunzi 24,000 waliofanya Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) mwaka jana katika kaunti za Pwani watalazimika kwenda kusomea ‘Bara’ kutokana na ukosefu wa nafasi katika shule za upili za eneo hilo.

Kulingana na takwimu zilizotolewa jana na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, zinaonyesha kuwa kaunti zote sita za Pwani; Kilifi, Mombasa, Kwale, Taita Taveta, Tana River na Lamu hazina nafasi kusajili wanafunzi wote waliofanya KCPE mwaka 2022.

Kaunti zote za Pwani zina jumla ya shule 443 za sekondari zilizo na uwezo wa kusajili wanafunzi 43,258 katika Kidato cha Kwanza.Kaunti ya Kilifi ina jumla ya shule 164 za upili zilizo na uwezo wa kusajili wanafunzi 31,258 katika Kidato cha Kwanza.

Lakini wanafunzi 41,470 walifanya mtihani wa KCPE katika kaunti hiyo. Hiyo inamaanisha kuwa wanafunzi 10,212 watalazimika kuelekea kaunti za ‘Bara’ kuendeleza masomo yao ya shule ya sekondari.

Wanafunzi 9,559 watakosa nafasi katika Kaunti ya Mombasa, Kwale (1,809), Taita Taveta (1,709), Tana River (803) na Lamu (496).

Jumla ya wanafunzi 85,078, nusu yao wakitoka jijini Nairobi, watalazimika kwenda kusomea katika kaunti jirani kutokana na ukosefu wa nafasi katika maeneo yao.Licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, Kaunti ya Nairobi ina shule 109 pekee za upili.

Licha ya kuwa na shule 449 za sekondari, Kaunti ya Kitui haitaweza kusajili wanafunzi 1,078 ambao sasa watalazimika kwenda kusomea katika kaunti jirani.

“Wizara itachukua hatua kwa kufanya mazungumzo na viongozi wa kaunti zisizo na shule za kutosha kuhakikisha kuwa madarasa zaidi ili kuepuka uhaba wa aina hii katika siku za usoni,” akasema Waziri wa Elimu.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni ya Crystal River yajizolea sifa kwa kutengeneza...

TIBA NA TABIBU: Glasi nane za maji kila siku zitakuongezea...

T L