• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 2:53 PM
TUJIFUNZE THAMANI YA NYUKI: Wanachohitaji wafugaji ni hamasisho na mafunzo kuhusu ufugaji nyuki

TUJIFUNZE THAMANI YA NYUKI: Wanachohitaji wafugaji ni hamasisho na mafunzo kuhusu ufugaji nyuki

NA SAMMY WAWERU

KIWANGO cha asali tunayozalisha nchini kikiwa chini ya asilimia 20, ni bayana nafasi ipo kwa wenye ari ya kuingilia ufugaji wa nyuki.

Takwimu hizo kwa mujibu wa Taasisi ya Ufugaji Nyuki Nchini, inaashiria mwanya mkubwa wa kuendeleza ufugaji nyuki.

Baringo, Makueni, Kitui na Kajiado ndiyo maeneo yanayoongoza katika uzalishaji wa asali Kenya, na Ezra Owiti kutoka shirika hilo anasema Kenya ina uwezo kuziba mwanya uliopo.

Kiwango kikubwa cha bidhaa hii huagizwa kutoka Tanzania, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Sudan.

“Wanachohitaji wafugaji na wenye ari, ni hamasisho na kupata mafunzo kuhusu ufugaji nyuki,” asema afisa huyu anayetoa huduma za mafunzo maalum.

Kando na kurina asali, mdau huyu anasema wafugaji wanapaswa kukumbatia mifumo ya uongezaji thamani nta akisisitiza kwamba mkondo huo ndio siri ya donge nono.

“Nta inayotokana na masega, ni malighafi kutengeneza mishumaa, sabuni, mafuta ya kujipodoa na shampoo, kati ya bidhaa nyingine. Uongezaji thamani una pesa,” aelezea.

Asali vilevile, inaweza kusindikwa kwa matunda na viungo vya vinywaji, Blossoms & Beehives ikikiri hatua hiyo inachochea bidhaa hiyo kuteka soko lenye ushindani mkuu.

“Covid-19 ilipotua nchini, wengi waligeukia asali na kuichanganya na viungo vyenye virutubisho kama vile ndimu kuongeza kinga dhidi ya Homa hiyo ya Corona,” asema Dorah James, mfanyakazi katika kampuni hiyo ya kibinafsi.

Kabla kuingilia ufugaji nyuki, unahimizwa kushirikisha Mamlaka ya Uhifadhi wa Mazingira Nchini (Nema) ili kutathmini usalama eneo unalolenga kuweka mizinga.

  • Tags

You can share this post!

Mudavadi apanda bei

Siri ya ufugaji nyuki ipo katika uongezeaji thamani

T L