• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:24 PM
UJASIRIAMALI: Ana magari ya wateja kulipia wayatumie kwa muda fulani

UJASIRIAMALI: Ana magari ya wateja kulipia wayatumie kwa muda fulani

NA MAGDALENE WANJA

BAADA ya kufanya biashara za aina mbalimbali, ikiwemo ya mitumba, Bw Simon Kibe aligundua kuwa kulikuwa na pengo katika biashara ya kukodisha magari ya kibiashara.

Baadhi ya marafiki zake ambao walikuwa katika biashara mbalimbali walimuelezea jinsi walitaka magari aya kutumia kwa muda mfupi ila hawakuridhika na baadhi ya magari yaliyokuwa yakipatikana ya kukodisha.

Alifanya utafitina akagundua kwamba biashara hio ingempa faida.

“Mnamo mwaka 2016, niliamua kujaribu biashara hiyo, na kufikia mwaka 2018 nilisajili biashara ya kukodisha magari na kuiita Kizusi Smartex Limited,” akasema Bw Kibe.

Kampuni hio inatoa huduma mbalimbali zikiwemo magari madogo, magari ya kifahari, madereva wa kukodishwa na magari ya kitalii.

Magari kwenye yadi. PICHA | MAGDALENE WANJA

Alipokuwa akianza kufanya biashara hio, alitegemea magari ya kukodisha ambapo aliwalipa wamiliki kila mwisho wa mwezi.

“Kufikia sasa nina magari ya wateja ambao hulipwa kila mwezi pamoja na magari yangu binafsi,” anaongeza Kibe.

Wateja hulipa kati ya Sh3,500 na Sh20,000 bei ambazo hutegemea aina na ukubwa wa gari ambalo mteja ananuia kulitumia.

Ofisi kuu ya kampuni hiyo iki katika mtaa wa Fedha, eneo la Embakasi jijini Nairobi.

Anasema lengo lao ni kuwa na wawekezaji zaidi katika kampuni ili kuwawezesha kupanua biashara na kuwafikia wateja katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi na miji mingine mikuu nchini.

  • Tags

You can share this post!

JURGEN NAMBEKA: Vijana wa Pwani wajifunze kuhusu utaalamu...

Mathare yafufuka na kuishangaza Gor KPL

T L