• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Mzio wa chakula kwa mtoto mchanga

UJAUZITO NA UZAZI: Mzio wa chakula kwa mtoto mchanga

NA PAULINE ONGAJI

MZIO wa chakula hasa kwa watoto ni tatizo la kawaida ambalo hukumba angalau kila mmoja wakati mmoja maishani.

Duniani, mzio wa chakula unasemekana kuathiri watoto wengi huku asilimia 40 wakiathirika kwa njia moja au nyingine.

Mzio kamili wa chakula ni mwitiko usio wa kawaida katika mfumo wa kingamwili baada ya kula chakula fulani.

Hujitokeza kupitia allergen kwenye chakula, viungo ambavyo vinachochea hali hii.

Kwa wingi viungo hivi huwa protini zinazokinza moto wakati wa upishi, asidi kwenye tumbo na vimeng’enya tumboni.

Allergen hizo hudumu kwenye ukuta wa utumbo, kuingia kwenye mfumo wa damu na kulenga viungo fulani mwilini na hivyo kusababisha mzio.

Mara nyingi mzio miongoni mwa watoto hutokea katika kipindi cha mwaka mmoja au miwili ya kwanza ya mtoto.

Japo mzio wa vyakula kama maziwa na mayai huisha mtoto anapozidi kukua, kuna ambao huendelea maishani. Litakuwa jambo muhimu kumpeleka mwanao hospitalini ili achunguzwe vilivyo.

Kumbuka kwamba kumnyonyesha mtoto pekee pasipo kumlisha chakula kingine katika miezi minne ya kwanza maishani husaidia kupunguza uwezekano wa kukumbwa na mzio wa maziwa katika miaka miwili ya kwanza.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Nyama ya mbuzi na viazi vilivyopondwa

BAHARI YA MAPENZI: Je, inafaa kutegemea watoto uzeeni?

T L