• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la mtoto kuvuja mkojo

UJAUZITO NA UZAZI: Tatizo la mtoto kuvuja mkojo

NA PAULINE ONGAJI

TATIZO la mtoto kuvuja mkojo laweza msababishia mzazi yeyote yule wasiwasi.

Lakini ukweli ni kwamba ni kawaida hata kwa mtoto aliye na umri wa zaidi ya miaka mitatu ambaye amefunzwa kuenda chooni kukumbwa na tatizo hili.

Kumbuka kwamba hata ikiwa mtoto ametimu umri huu, huenda hajapata uwezo wa kudhibiti kibofu chake, na hivyo ana nafasi hadi kufikia miaka sita ili kufanya hivyo.

Hata hivyo kuna masuala ambayo yaweza chochea mkojo kuanza kuvuja kama vile wasiwasi, kubadilishwa mazingira, hali ya familia, dhuluma, kuvimba tumbo, kisukari, maambukizi ya mfumo wa mkojo (Urinary Tract Infection), kutumia kafeini, kulala usingizi wa pono au ikiwa kuna matatizo ya kibofu.

Ikiwa mwanao anakumbwa na shida hii, litakuwa jambo la busara kumpeleka akaguliwe na daktari ambapo chunguzi kadhaa zitafanywa kubaini iwapo kuna maradhi mengine.

  • Tags

You can share this post!

JUNGU KUU: Kibarua cha Raila na Uhuru kuokoa Azimio

Wito serikali isambaze chakula kwa wakazi wa Ganze na Bamba

T L