• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Umri sahihi wa mtoto kuanza kukaa mwenyewe

UJAUZITO NA UZAZI: Umri sahihi wa mtoto kuanza kukaa mwenyewe

NA PAULINE ONGAJI

KUNA wazazi wanaokumbwa na wasiwasi watoto wao wanapokawia kujihimili au kukaa. Lakini hili sio jambo ambalo linapaswa kukupa hofu.

Kwa kawaida watoto huanza kujifunza kujihimili wakiwa katika umri wa kati ya miezi minne na sita na kuanza kukaa pasipo usaidizi. Kuna baadhi ya watoto ambao hujifunza mapema na kunao hujifunza baadaye.

Katika umri wa miezi saba, bado mtoto ana muda wa kujifunza kukaa. Mtoto akitimu miezi tisa ilhali hawezi keti chini, sasa hapo ndipo unapaswa kuanza kuwa na wasiwasi.

Baadhi ya masuala ambayo huenda yakamsababisha achelewe ni pamoja na mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake, utapiamlo, maradhi ya matege (rickets) yanayotokana na viwango vya chini vya vitamini D, kupuuzwa, matatizo ya kijenetiki, au shida za neva au misuli.

Ikiwa mtoto anaweza dhibiti shingo lake vyema na viungo vyake vina mwendo kiasi kwamba anaweza jisukuma au kujipindua, basi yuko tayari kuanza kujifunza kukaa.

Mwanzoni mtoto anapaswa kuhimiliwa anapoketi chini, na muda unavyozidi kusonga, punguza vihimili hadi atakapoweza kukaa mwenyewe bila usaidizi.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge wa Sirisia John Waluke atoka gereza la Kamiti

MAPISHI KIKWETU: Kuimarisha ladha ya chapati za maji

T L