• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
MAPISHI KIKWETU: Kuimarisha ladha ya chapati za maji

MAPISHI KIKWETU: Kuimarisha ladha ya chapati za maji

NA PAULINE ONGAJI

CHAPATI za maji ni vyakula sahili na rahisi kutayarisha unapoandaa kiamsha kinywa.

Hata hivyo iwapo haujui kuandaa chakula hiki huenda usipendezwe sana na ladha yake. Lakini kuna mbinu za kuimarisha ladha kama vile:

•Kuongeza siagi: Kiungo hiki huongezwa katika kinyunya pamoja na sukari, mayai, maziwa na unga ili kuimarisha ladha unapoandaa.

•Ndimu: Uchachu wa ndimu huimarisha ladha dufu ya chakula hiki. Baada ya kuzipika changanya maji ya ndimu pamoja na sukari katika kikombe na kuzinyunyizia kisha kuandaa mara moja.

•Asali: Kama maji ya ndimu, asali hunyunyiziwa juu ya chapati hizi zikishakuwa tayari kabla ya kuandaliwa.

•Kakao. Mbali na kuimarisha ladha, rangi yake ya kahawia hukupa hamu ya kutaka kula chakula hiki. Kiungo hiki huchanganywa na unga wa ngano na kuchungwa kisha huongezwa kwenye mayai na maziwa kabla ya mapishi kuanza.

•Unga wa njugu zilizokaangwa: Huchanganywa pamoja na unga wa ngano.

•Chembe za mkate: Hunyunyizwa kwenye kinyunya kabla ya mapishi kuanza.

•Shira: Chapati za maji zaweza liwa pamoja na shira iliyoundwa kwa mchanganyiko wa sukari, maji, iliki, mdalasini na pilipili kali.

  • Tags

You can share this post!

UJAUZITO NA UZAZI: Umri sahihi wa mtoto kuanza kukaa...

MALEZI KIDIJITALI: Athari mseto za matumizi ya dijitali kwa...

T L