• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
ULIMBWENDE: Tumia foronya za satini na silki kutunza nywele zako unapolala

ULIMBWENDE: Tumia foronya za satini na silki kutunza nywele zako unapolala

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WANAWAKE wengi hutumia pesa nyingi katika kununua bidhaa za nywele lakini bado unaona matokeo sio mazuri au yanachelewa kudhihirika.

Hii inaweza kuwa ni kutokana na kitambaa cha mto au shuka unayolalia. Mito au mashuka ya pamba huwa yananyonya mafuta kwenye nywele lakini pia kuzifanya ziwe nyepesi na kuzifanya zigawanyike pembeni.

Lakini kwa upande wa kitambaa cha satini au silki, kipo nyororo na kinaweza kukuondolea hayo matatizo yote. Hivyo, unashauriwa kutumia mito ya silki/satini yenye ubora wa hali ya juu.

Hakuna tofauti ya kutumia kitambaa kimoja kati ya hivyo viwili. Tatizo tu ni kwamba silki ni ya bei ghali kuliko satini.

Ni vigumu kupata uzuri wako usingizi wakati unasisitizwa kuhusu jinsi nywele zako zitakavyoonekana asubuhi. Tamaduni za urembo sio tu kwa ngozi yetu, bali pia nywele.

Silki na satini husaidiaje katika uboreshaji wa nywele zako?

Zinafanya nywele kuwa na afya

Kwa namna moja au nyingine mito ya silki au satini inafanya nywele kuwa na afya. Foronya za aina hii hazinyonyi mafuta kwenye nywele na kufanya nywele iwe na unyevu. Kama unalalia mito ya pamba, unaweza kuwa umekumbana na hali hii – umeenda saluni umetengeneza nywele zako na kupaka mafuta lakini ukiamka siku inayofuata nywele zimechachamaa. Hali hii husababishwa na kitambaa cha mto kunyonya mafuta katika nywele zako.

Kufanya nywele zako zisifungamane

Wakati ukilalalia mito yenye kitambaa cha pamba, nywele zako zinafungamana na kukupa kazi ya ziada wakati wa kuchana. Hii ni tofauti na ukilalia kitambaa cha ama silki au satini kwa sababu huwa laini na hivyo kuepusha nywele zako kufungamana. Hii itakupa urahisi wakati wa kuchana nywele.

Kuepusha kukatika kwa nywele

Mito yenye kitambaa cha silki haivuti nywele ukilala tofauti na pamba. Silki yenyewe inahifadhi mafuta, ipo nyororo na haivuti wala kufanya nywele zishikane.

Hulinda uso wako

Nywele zinaweza kuchukua aina mbalimbali za vimelea siku nzima. Ni muhimu kutoosha nywele kila siku ili kuhifadhi mafuta ya asili na yenye kinga ndani yake. Kulalia foronya za satini kunasaidia kuzuia vimelea hivi kuingia. Vikiingia nweleni, vinaweza kusababisha chunusi.

  • Tags

You can share this post!

Faida za mafuta ya mbarika yaani castor oil

Sonko amalizika kisiasa

T L