• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Umuhimu wa vitamini E

Umuhimu wa vitamini E

Na MARGARET MAINA

[email protected]

VITAMINI E kwa kawaida ni ya asili ya mafuta mafuta.

Hupatikana katika mafuta ya mimea, nafaka na mboga za majani

Vitamini E hufanya kazi kama anti-oxidant inayosaidia kupunguza kiwango cha seli kuharibika na kufa. Hii ina maana anti-oxidant hulinda seli dhidi ya kemikali haribifu.

Vitamini E huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali mwilin hasa:

  • katika tishu za mafuta
  • moyo
  • misuli
  • kwenye damu
  • mafuta yatokanayo na mimea na mbogamboga
  • viazi vitamu
  • kiini cha yai
  • ini
  • maharage jamii ya soya
  • maziwa

Kukaanga au kuchemsha au kugandisha kwenye jokovu kwa muda mrefu husababisha vyakula kupoteza kiwango fulani cha Vitamini E.

Matatizo yatokanayo na upungufu wa Vitamini E

Ikizingatiwa kwamba Vitamini E huwa tele kwenye vyakula, upungufu wa mwanzo kabisa wa Vitamini E ni nadra kutokea.

Lakini imeripotiwa kutokea kwa watoto waliozaliwa chini ya uzani wa kawaida ambao hupewa maziwa ya ng’ombe yenye kiwango kidogo cha Vitamini E na kwa wenye matatizo ya utumbo.

Dalili ambazo huashiria upungufu wa Vitamin E ni kama zifuatazo:

  • Upungufu wa damu (Haemolytic anaemia)
  • Matatizo yahusuyo mfumo wa kinga ya mwili
  • Matatizo yahusuyo mfumo wa fahamu
  • Matatizo ya ugandaji wa damu mwilini
  • Mafuta mengi kwenye damu

Matumizi ya Vitamini E kitaalamu

  • Kujikinga na matatizo yatokanayo na upungufu wa Vitamini E
  • Matibabu ya magonjwa ya moyo
  • Matibabu ya magonjwa ya akili na uelewa
  • Huboresha kinga ya mwili kwa wazee
  • Husaidia kupunguza dalili zinazotokea kabla ya kupata hedhi
  • Matibabu ya maumivu ya miguu
  • Matibabu ya ngozi
  • Kwa wenye matatizo ya kutembea
  • Kwa walio na ugonjwa wa kisukari
  • Pumu na mzio au allergy nyinginezo.
  • Homa ya ini

TANBIHI: Mama mjamzito anaweza kupewa Vitamini E kama ana historia ya mimba kutoka mara kwa mara.

You can share this post!

Baadhi ya wanasoka wa haiba kubwa waliowahi kuondoka katika...

PSG kuweka mezani Sh13 bilioni kwa ajili ya Richarlson...