• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Uswahilini sihami, niende wapi na ndo nimeshafika!

Uswahilini sihami, niende wapi na ndo nimeshafika!

NA SIZARINA HAMISI

USWAHILINI sihami, tena siondoki kamwe.

Nahamaje mahali ambako kila siku najipatia burudani ya moyo, burudani ya maneno na wakati mwingine burudani ya mwili?

Muulize mwanamume yeyote anayeishi huku kwetu, atakueleza tabia moja mbaya wanayojisifu nayo mitaani ni kwamba raha ya uswazi ukitandika msichana wa wenyewe, tena umtandike vizuri hadi anyooke lazima ataenda kumsimulia rafiki yake.

Huyo rafiki yake naye atataka aje kuhakikisha, naye utajikuta unamtandika vya kutosha, akitoka hapo ataenda kumsimulia dada yake muuza mkahawa, naye atakuja mbio kuhakikisha na utaishia kumchapa, yaani inakuwa ni foleni na usipoangalia unaweza kujipata unachapa ukoo mzima na marafiki zao wote.

Ukiishi huku kwetu, maisha yako sio siri, kila mkazi wa maeneo haya atataka ajue maisha yako. Kama maisha yako ya kuunga unga kama suruali iliyotoboka, basi ukipata shida hawatakuacha, watakutafuatilia hadi mtangazaji wa redioni ili upatiwe msaada ilimradi usiishie kuathirika.

Lakini pia kama maisha yako yametulia na pesa ya mboga sio shida, basi uishi kwa heshima. Ukienda kwenye msiba, kula hata kama hauna njaa. Ukiwekewa sinia la chakula, ushirikiane na wenzako, usijifanye kuinua mdomo wako juu na kuanza kuongea matope, utadhalilishwa.

Kwani usipokula watakuweka alama na siku itokee nawe ufikwe na dhoruba fulani na ukaribishe watu wa mtaani, nao watakuja waketi, wakuangalie usoni na wapandishe midomo juu kama wamenusa harufu isiyofaa.

Huku kwetu kuvaliana nguo ni kitu cha kawaida. Unaweza kununua khanga na kuwapa mashosti wakutolee upya, kwamba waivae kwa muda fulani kisha wakurudushie uendelee nayo.

Huku tunashirikiana kwa shida na raha. Kama huna chakula cha kuwapa watoto usishangae habari zitaenea na sahani za chakula zitaingia, tena za kutosha.

Tunapendana na tunajaliana. Isipokuwa usijaribu uwavuruge. Ukitenda yasiyofaa na yasiyoendana na maisha yetu, hapo ndipo utaonja chungu ya uswazi. Utavurugwa pia kwa maneno ambayo wenyewe wanaita kuchamba, kwamba wanakuchambua kuanzia kichwani hadi miguuni kiasi kwamba unaweza ukajiona uko mtupu.

Wakusasambue na wakati mwingine wakuitie hadi wapuliza matarumbeta na mtaa unafungwa ili kukufikishia ujumbe vizuri.

Hivyo sielewi na nashindwa kutambua pale ninapoambiwa huenda siku moja nitahama huku Uswahilini. Niende wapi mwenzenu? Ndio nimeshafika hivyo!

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

BAHARI YA MAPENZI: Je, inafaa mke kushika hatamu nyumbani?

WALIOBOBEA: Ndwiga, waziri mtulivu aliyechapa kazi vyema

T L